Skip to main content

JUMUIYA YA WAZAZI MPANDA YAHAMASISHA UPENDO, MEYA AHIMIZA USAFI WA MAZINGIRA

Na Daniel Gahu - Katavi.

JUMUIYA YA WAZAZI MPANDA YAHAMASISHA UPENDO, MEYA AHIMIZA USAFI WA MAZINGIRA

Na Daniel Gahu - Katavi.

Jumuiya ya Wazazi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi, imeadhimia mambo mbalimbali wakati wa Baraza kuu la Jumuiya hiyo, lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chama hicho wilayani Mpanda, huku lengo kuu la kikao hicho ni kuongeza chachu ya mwitikio wa wajumbe kutoka Jumuiya hiyo kuhakikisha wanahudhuria kwa wingi katika kilele cha maadhimisho ya Jumuiya hiyo ngazi ya Taifa jijini Mwanza.

Wakijadili wakati wa Baraza hilo, wajumbe wa Jumuiya hiyo wameafikiana kuhakikisha wanahudhuria kwa wingi katika kilele cha maadhimisho ya Jumuiya ya Wazazi ngazi ya Taifa yatakayofanyika ndani ya Jiji la Mwanza.

"Niwaombe sana ndugu zangu kuhakikisha kila mmoja anajipanga kuhudhuria maadhimisho ya Jumuiya yetu yatakayofanyika Mkoani Mwanza" amesema Jimotoli Jilala Katibu mtendaji wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Mpanda.

Akizungumza wakati wa Baraza hilo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Charles Filipo amewashukuru wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Mpanda kwa kumuunga mkono na kujitoa kwa hali na mali kuhakikisha anafanikiwa kuwa Meya wa Manispaa kutoka katika Jumuiya hiyo.

"Niwaombe sana muendelee kuniunga mkono, kwani majukumu niliyonayo kwa hivi sasa nimakubwa mnoo, ninaomba ushirikiano wenu, ninaomba dua zenu ili niweze kutumika vyema katika Baraza hili na niweze kuiheshimisha Jumuiya ya Wazazi".

"Ninajua kabisa kijana wenu mnanipenda" "na mimi niseme tu nina wapenda zaidi" niko tayari kushirikiana na viongozi wote wa Jumuiya ya Wazazi, kwa ngazi zote na kwa nafasi zote, Ninaomba mnapokuwa na jambo mimi kijana wenu mnaweza kunishirikisha wakati wowote kwani niko tayari kushirikiana nanyi kwa maslahi mapana ya Jumuiya yetu ya Wazazi." Amesema Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda.

Amesisitiza kuwa kwa nafasi yake aliyonayo atawajibika kwa usawa katika Kata zote kumi na tano za wilaya ya Mpanda huku akihakikisha kutokuwa Meya wa makundi kwa kufahamu moja ya majukumu ya Kiongozi ni pamoja na kuunganisha watu.

Aidha ametoa wito kwa wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi kuhakikisha wanazingatia usafi wa mazingira katika maeneo yao kwa kuwa mfano wa kuigwa katika maeneo wanayoishi huku akiwataka wajumbe wa Jumuiya hiyo kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana ndani ya wilaya hiyo ya Mpanda.

"Itakuwa ni jambo la ajabu sana kumuona mjumbe au Kiongozi wa Jumuiya ya Wazazi anakuwa mstari wa mbele kwa kutokufanya usafi wa mazingira katika eneo lake, hivyo niwaombe mkawe mabalozi na mfano wa kuigwa kwa kufanya usafi katika maeneo yenu" amesisitiza Mstahiki Meya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Mpanda, amewataka wajumbe wa Jumuiya hiyo kuendelea kudumisha upendo na mshikamano ili kuhakikisha Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Mpanda inastawi na kuwa chachu ya mafanikio ya kila mmoja katika kufikia malengo yake ya kisiasa.

"Ningependa sana msizodoane zodoane, kama itatokea mmoja wenu amewakwaza basi muonyane kwa upole, itakuwa ni ajabu watu kuwaona wazazi ambao ndio waliobeba maono ndani ya Chama mnakuwa na migogoro hilo halitakiwi" amesema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Mpanda wakati wa kufunga kikao cha Baraza la Jumuiya ya Wazazi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.