Skip to main content

JUMUIYA YA WAZAZI KATAVI YAADHIMISHA WIKI KWA KUWATEMBELEA WAGONJWA

Na Daniel Gahu - Katavi.

JUMUIYA YA WAZAZI KATAVI YAADHIMISHA WIKI KWA KUWATEMBELEA WAGONJWA
Studio Narration JAMBO FM

JUMUIYA YA WAZAZI KATAVI YAADHIMISHA WIKI KWA KUWATEMBELEA W...

0:00 --:--

Na Daniel Gahu - Katavi.

Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi imeadhimisha kwa kishindo wiki ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi kwa kutembelea wagonjwa katika hospital ya Halmashauri ya Nsimbo iliyopo wilaya ya Mpanda, ambapo wametoa misaada ya sabuni kwa wagonjwa katika Wodi ya wanawake waliojifungua pamoja na wodi ya watoto.

Maadhimisho hayo yamefanyika Leo tarehe 07/05/2026 na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Katavi ndugu Evarist Simon Mnyere ambaye amesema katika kuimarisha Chama na Jumuiya ili kuweza kutambua majukumu yake, ambapo Jumuiya ndizo zinazoimarisha Chama kiutendaji.

Ameendelea kusema Jumuiya ya Wazazi kazi yake kubwa ni masuala ya malezi, elimu,na Afya ambapo hushirikiana na wadau wengine ili kuangalia nini kinaendelea katika vituo mbalimbali vya afya.

"Mimi ni mzaliwa wa kijiji cha Sungamila, kwakweli maendeleo ni makubwa sana kwani hapo awali hakukuwa na hospital katika eneo hili lakini leo nimeshangaa kuiona hospitali kubwa namna hii na iliyosheheni vifaa tiba pamoja na wahudumu wa afya wa kutosha, kwa kweli itoshe kutoa pongezi kwa chama na Serikali hii ya awamu ya sita," amesema Mnyere.

Aidha amesema, imechukua miaka mingi sana kuona vituo vya afya viko karibu karibu kama ilivyo hivi sasa kwani kipindi cha nyuma tulikuwa tunasafiri umbali mrefu kuzitafuta huduma za afya jambo ambalo lilichangia vifo kwa wakina mama wajawazito na watoto kutokana na ukosefu wa huduma kwa ukaribu.

"Ni jukumu la Jumuiya hii ambayo ni Jumuiya mama katika kusimamia mambo mengine ili kwenda katika uelekeo unaoeleweka hasa katika swala zima la malezi na maadili kwa watoto na watu wazima kwa ujumla," ameongeza Mnyere.

Pia amewataka watumishi wa Hospitali hiyo ya halmashauri ya Nsimbo kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia misingi ya maadili ya kazi hiyo ili wananchi waweze kuridhika na kufurahia huduma zinazopatikana katika hospitali hiyo, kwani kwa kufanya hivyo imani ya wananchi kwa Serikali itaongezeka maradufu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa mbele ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya wazazi ndugu Evarist Simon Mnyere, imebainisha hospitali hiyo ina jumla ya watumishi 126 wa kada mbalimbali ya afya na utawala ambapo inahudumia idadi ya watu takribani laki mbili wa halmashauri hiyo pamoja na wa maeneo jirani.

Ambapo katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya na zenye gharama nafuu na zinazofikika kwa wananchi wote, hospitali imeboreshwa kwa kuwa na majengo kumi na nne muhimu yanayowezesha utoaji wa huduma kwa ufanisi.

Pia jengo la utawala, jengo la dharula, jengo la wagonjwa wa nje, maabara, kitengo cha mionzi, jengo la wazazi, jengo la kuhifadhia maiti na majengo mengineyo ambayo yameboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.