Skip to main content

JUMUIYA YA WAZAZI CCM YASITITIZA MALEZI YA WATOTO NGAZI YA FAMILIA.

Na William Bundala, Kahama - Shiyanga

JUMUIYA YA WAZAZI CCM YASITITIZA MALEZI YA WATOTO NGAZI YA FAMILIA.

Na William Bundala, Kahama - Shiyanga

Chama cha Mapinduzi kimesisitiza umuhimu wa malezi kwa watoto kuanzia ngazi ya familia na kwamba moja ya majukumu yay a jumuiya ya wazazi ya chama cha Mapinduzi kuhakikisha jamii inakuwa na malezi bora kila wakati.

Hayo yamebainishwa na Katibu wa Jumuia ya Wazazi Taifa, Ally Hapi katika semina ya wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) iliyofanyika manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Hapi amesema kwa Malezi mema yanaanza ndani ya familia hivyo ni wajibu w chama kupitia jumuiya ya wazazi kuikumbusha jamii kuhusu malezi ingali mapema ili taifa letu  liwe na vijana wenye maadili na Uzalendo.

“Wazazi niwaombe sana nyinyi ndio walimu wa kwanza mnapokuwa nyumbani,hakikisheni mnawapa mafunzo na malezi bora watoto wenu kuanzia ngazi ya familia,hii itasaidia vijana wetu kuwa na maadili mema Pamoja kuwa wazalendo katika taifa.” Amesema Hapi.

Sambamba na hayo Hapi ametoa wito kwa wanachama wa chama hicho hususan waliopo kwenye jumuiya hiyo kuendelea kutoa elimu ya malezi kuanzia ngazi za viviji,kata,Wilaya hadi taifa.

“Sisi kama jumuiya tuna wajibu mkubwa wa kuwafikia wananchi na kuzidi kutoa elimu ya malezi kwa watoto wetu,hatuwezi kukwepa sababu ni moja ya jukumu na wajibu wa Jumuiya ya wazazi ya chama cha Mapinduzi” Amesisitiza Hapi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  Mkoa wa shinyanga Mabala Mlolwa amesema chama kimeendelea kushirikiana vyema na serikali kutatua Migogoro ya wananchi katika Nyanja zote.

“Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga kimeendelea kushirikiana vyema na serikali katika kutatua migogoro ya wananchi katika Nyanja zote za Elimu,Afya,Miundombinu Pamoja na kuwafikia wanachi ili kujua changamoto walizonazo katika maeneo yao” Amesema Mabala.

Awali akitoa salamu za jimbo Mbunge wa jimbo la Kahama mjini Benjamini Ngayiwa amezungumzia miradi inayoendelea katika manispaa ya Kahama ikiwemo ujenzi wa Barabara za lami,ujenzi wa chujio la maji Pamoja na stendi mpya ya mabasi Pamoja na ujenzi wa masoko.

“Mheshimiwa mgeni rasmi sisi Kahama tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea miradi mingi ya maendeleo,ambapo tunaendelea na Ujenzi wa barabara zetu kwa kiwango cha lami,Ujenzi wa chujio la maji kutoka Buzwagi Pamoja na ujenzi wa Soko la sango na stendi mpya yam abasi” Amesema Ngayiwa.

Semina hiyo imelenga  kuwajengea uwezo viongozi na wanachama wa CCM Wilaya ya Kahama katika utekelezaji wa majukumu yao ya msingi, ikiwemo kutatua kero za wananchi na kudumisha umoja wa chama.

Wanachama na viongozi walioshirikia semina wameahidi kupeleka ujumbe huo kwenye matawi na kata ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na migogolo inatatuliwa kwa wakati.

Katibu wa Jumuia ya Wazazi Taifa, Ally Hapi, amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na wanachama kutimiza wajibu wao kwa kuwatumikia wananchi na kutatua migogolo inayowakabili katika maeneo yao.

Hapi ameyabainisha hayo kufuatia semina ya wanachama wa CCM Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga iliyofanyika katika Ukumbi wa Malex, Kahama.

Kiongozi huyo ngazi ya Taifa pia amesisitiza umuhimu wa malezi kwa watoto kuanzia ngazi ya familia, Amesema moja ya majukumu makuu ya Jumuia ya Wazazi ni kuhakikisha malezi bora ndani ya jamii.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa shinyanga Ndg Mabala Mlolwa amesema chama kimeendelea kushirikiana vyema na serikali kutatua Migogoro ya wananchi.

Semina hiyo imelenga  kuwajengea uwezo viongozi na wanachama wa CCM Wilaya ya Kahama katika utekelezaji wa majukumu yao ya msingi, ikiwemo kutatua kero za wananchi na kudumisha umoja wa chama.

Wanachama na viongozi walioshirikia semina wameahidi kupeleka ujumbe huo kwenye matawi na kata ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na migogolo inatatuliwa kwa wakati.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.