Skip to main content

JUMA MBARONI KWA KUIDANGANYA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MANYARA

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Salimu Juma amelazimika kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, baada ya kubainika kutoa taarifa za kupotosha mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kuhusu mgogoro wa nyumba kati yake na baba yake mzazi.

Salimu Juma anatuhumiwa kumfukuza baba yake mzazi, Mzee Juma Salimu mwenye umri wa miaka 85, kutoka kwenye nyumba ambayo inadaiwa kujengwa na baba huyo, huku kijana huyo akidai kuwa nyumba hiyo ni mali yake aliyopewa tangu akiwa na umri wa miaka mitano.

Kutokana na mgogoro huo, Mzee Juma Salimu amelazimika kuondoka katika nyumba hiyo na kwenda kuishi kwa muda katika nyumba ya mtoto wake wa kike.

Baada ya suala hilo kufikishwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Kamati ya Ulinzi na Usalama ilifika eneo la tukio ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Queen Sendiga kwa lengo la kusikiliza pande zote mbili na kutafuta suluhu ya mgogoro huo.

Hata hivyo, wakati wa usikilizwaji wa suala hilo, Salimu Juma ambaye awali alikuwa amewahi kufikishwa katika ngazi ya serikali ya mtaa, alidai kuwa hafahamu chochote kuhusu mgogoro huo, jambo lililoibua maswali kwa kamati hiyo.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Manyara alitoa amri ya kushikiliwa kwa Salimu Juma na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi kuhusu tuhuma zinazomkabili.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.