Skip to main content

JUKWAA MAENDELEO YA USHIRIKA DODOMA KUBORESHA MAISHA YA WANANCHI

Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoa wa Dodoma limezinduliwa rasmi kwa kutoa Hundi ya kiasi cha Shillingi Milioni 14,690,200 kwa Wanafunzi 29 wa Vyuo vikuu vya Dodoma ikiwemo UDOM, Mipango na Hombolo.

JUKWAA MAENDELEO YA  USHIRIKA DODOMA KUBORESHA MAISHA YA WANANCHI

Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoa wa Dodoma limezinduliwa rasmi kwa kutoa Hundi ya kiasi cha Shillingi Milioni 14,690,200 kwa Wanafunzi 29 wa Vyuo vikuu vya Dodoma ikiwemo UDOM, Mipango na Hombolo.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika Mei 29, 2026, Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Dodoma, Joseph Chitinka, amesema jukwaa hilo ni sehemu ya kuimarisha mshikamano na kuhakikisha ushirika unachangia kuboresha maisha ya wananchi, hususani wanafunzi kutoka familia zenye mazingira magumu.

Vyama vya Ushirika mkoa wa Dodoma limezindua rasmi Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Dodoma likilenga kuimarisha utekelezaji wa misingi ya ushirika, hususani msingi wa saba unaohusu kusaidia jamii na makundi yenye uhitaji.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo la Ushirika  Ibrahim  Sumbe, amesema hatua hiyo ni katika kuimarisha uhusiano wa Vyama vya Ushirika na  kurudisha faida ya utendaji  Jamii pamoja.

Maadhisho ya Jukwaa hilo yataendelea kwa ratiba nyingine ikiwemo Bonanza la Michezo pamoja na Mkutano wa majadiliano ya masuala ya Ushirika June 5-6, 2026 Jijini Dodoma.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.