Skip to main content

JUKWAA LA USHIRIKA SHINYANGA LAPELEKA TABASAMU KWA WATOTO YATIMA

Na William Bundala-Kahama Shinyanga

JUKWAA LA USHIRIKA SHINYANGA LAPELEKA TABASAMU KWA WATOTO YATIMA

Na William Bundala-Kahama Shinyanga

Kuelekea Jukwaa la Ushirika 2026  Kamati kuu ya jukwaa hilo mkoa wa Shinyanga limetembelea na kutoa misaada katika vituo vya kulelea watoto yatima cha Zaqahana na New hope  vilivyopo kata ya Kagongwa na Zongomela.

Wakikabidhi misaada hiyo Mwenyekiti wa jukwaa hilo mkoa wa Shinyanga Emmanuel Nyambi amesema kuwa wanatekeleza msingi wa wa saba wa Ushirika kila mwaka kwa kurudisha kwa jamii.

"Leo tumetembelea vituo hivi kwa lengo ka kutoa msaada kwa watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto yatima ikiwa ni utekelezaji wa Msingi wa saba wa ushirika kurudisha kwa jamii" Amesema Nyambi.

Nyambi ameongeza kuwa wametoa misaada mbalimbali ikiwemo Mahindi, Mchele, Unga, Sukari pamoja na vinywaji vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni mbili na elfu kumi na nane.

"Tumefanikiwa kuleta mahitaji yote muhimu vikiwemo chakula,Vinywaji na mahitaji mengine vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni mbili na elfu kumi na nane ambazo zimetolewa na jukwaa la ushirika Mkoa wa Shinyanga.

Katika hatua nyingine Nyambi ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga hususan waliopo manispaa ya Kahama kujitokeza kwa wingi kwenye jukwaa la ushirika la mkoa ambalo linatarajia kufanyika manispaa ya Kahama.

"Nitoe rai kwa wana Shinyanga wote kujitokeza kushiriki katika jukwaa la ushirika ambalo linafanyika hapa manispaa ya Kahama siku ya kesho june 5" Amesema Nyambi.

Awali wakizungumza wakati wakipokea msaada huo Mkurugenzi wa kituo cha New hope Seleman Juma na Meneja wa kituo cha Zaqahana Abdul Magayo wamewashukuru wana kamati wa jukwaa la ushirika kwa msaada huo na kwamba utasaidia kwa kiasi kikubwa upande wa chakula kwa watoto.

"Tunashukuru sana Kamati ya jukwaa la ushirika kwa msaada huu,vituo vyetu vinakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula lakini kwa msaada huu tunaamini utawasaidia watoto wetu kwa kiasi kikubwa," Wamesema wasimamizi hao.

Jukwaa la Ushirika mkoa wa shinyanga linatarajia kufanyika kesho manispaa ya Kahama likiwa na kauli mbiu isemayo linda ushirika, Chagua uadilifu.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.