Skip to main content

JUKUMU LA KUVIKABILI VITENDO VYA UKATILI NI LA KILA MMOJA - MHA. MAHUNDI

Na Faustine Kasala - Kigoma.

JUKUMU LA KUVIKABILI VITENDO VYA UKATILI NI LA KILA MMOJA - MHA. MAHUNDI

Na Faustine Kasala - Kigoma.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhandisi Marryprisca Mahundi, ameitaka jamii ya Mkoa wa Kigoma kuungana kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Akizungumza katika kikao maalumu kilichofanyika mkoani Kigoma kwa lengo la kujadili hali ya ukatili wa kijinsia na kuweka mikakati ya kuhakikisha mkoa huo unabaki salama, Mhandisi Mahundi amesema ukatili wa kijinsia unadhoofisha ustawi wa jamii na kuathiri maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

"Nitumie nafasi hii kuwakumbusha kuwa jukumu la kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ni la kila mmoja na kwa Takwimu za kiwango cha hali ya ukatili kwa makundi ya wanawake na hasa watoto hapa mkoani kigoma zipo juu sana hivyo nawaomba kila mmoja wetu atimize wajibu wake katika kukabiliana na hali hii," alisema Mhandisi Mahundi.

Aidha Mahundi amesema Serikali imeboresha Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia, ikiwemo ukatili unaofanyika kwa njia ya mtandao kwa kusambaza madawati ya jinsia katika maeneo mbalimbali, hususan masoko na stendi kuu za mabasi, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa waathirika na kuongeza ufanisi wa utoaji wa haki.

Akiwasilisha taarifa kuhusu hali ya ukatili wa kijinsia mkoani humo, Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Kigoma, Michael Mjema, amesema makosa yanayoripotiwa mara kwa mara ni pamoja na ubakaji, ulawiti, shambulio la kingono na kutelekeza familia.

Ameongeza kuwa wanawake, watoto na wazee ndio wanaoathirika zaidi na vitendo hivyo, huku Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Kigoma, Bi. Efetha Msiga, amesema takwimu za kipindi cha Januari hadi Juni 2026 zinaonesha kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na Kasulu TC zimeongoza kwa kuwa na matukio mengi ya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto.

Bi! Efetha ameongeza kuwa wanaume wanatajwa kwa kiwango kikubwa kuwa wahusika wa vitendo hivyo, na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano wa jamii katika kuzuia na kutoa taarifa za matukio ya ukatili kwa mamlaka husika.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.