Na Irene Kishiwa - Chumba cha Habari
Jeshi la Polisi nchini, limesema Taifa linaliwalinda Wanawake na Watoto kwa kujenga msingi imara wa amani na maendeleo, hivyo kila hatua inayochukuliwa katika kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia na dhidi ya watoto, ni uwekezaji kwa mustakabali wa Taifa .
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP) Camilius Wambura ameyabainisha hayo leo July 31, 2026 wakati akifunga mkutano wa dawati la jinsia na ulinzi wa mtoto wa mwaka 2025/2026 uliowakutanisha watendaji wa madawati ya jinsia na watoto zaidi ya mia tano kutoka Tanzania bara na Zanzibar uliofanyika jijini Dodoma.

Amesema, katika kipindi cha mwezi July,2025 hadi June 2026 utekelezaji wa shughuli za madawati umekuwa na mafanikio makubwa yanayo onesha uratibu wa huduma kati ya Taasisi mbalimbali,kuongeza ufanisi katika hatua za awali za uokoaji na kuchangia kujenga Imani ya wananchi kwa mifumo ya haki jinai.
“Mafanikio yanayoonekana leo si ya jeshi la polisi bali ni matokeo ya dhamira, ushirikiano na uwajibikaji kwa kila mdau aliyeshiriki katika safari hii na kwamba jeshi la polisi litaendelea kuimarisha uwezo wa watendaji wake kuboresha matumizi ya teknolojia, kuendeleza ushirikiano na wadau mbalimbali,"
na kusogeza huduma zaidi kwa jamii na dhamira ya jeshi la polisi ni kuhakikisha kuwa hakuna mwananchi atakayeshindwa kupata huduma kutokana na hofu,umbali au ukosefu wa taarifa," lisema IGP Wambura.

Aidha, Wambura pia ameizindua kitabu cha Mwanafunzi na muongozo wa Mwalimu kwa somo la jinsia na ulinzi wa mtoto, muongozo wa Mwalimu, Polisi Jamii na kituo kipya cha kutoa huduma ya mawasiliano cha kupinga ukatili wa kijinsia na kusema uwepo wake ni hatua muhimu katika kuongeza upatikanaji wa huduma ya haraka kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia.
Amesema, Wananchi pia wanatakiwa kutoa taarifa kwa haraka na kuimarisha mawasiliano na huduma kwa jeshi la polisi.
Mkutanao huo, ulinzishwa mwaka 2019 na kufanyika kama jukwaa muhimu na kutathmini utekelezaji wa majukumu, kujengeana uzoefu na kuweka mikakati ya kuimarisha huduma kwa wananchi na kwa mwaka huu umebebwa na kauli mbiu ya usawa wa kijinsia ulinzi wa mtoto ni msingi wa amani, haki na maendeleo.
Discussion
Reader comments
0 contributions