Skip to main content

JAMII YATAKIWA KUWA MAKINI KATIKA MALEZI YA WATOTO IKUNGI

Jamii imetakiwa kuwa makini katika malezi ya watoto, kwa kuhakikisha wanapewa malezi bora, uangalizi na maadili yanayowawezesha kukua katika mazingira salama na kujenga mustakabali wao.

JAMII YATAKIWA KUWA MAKINI KATIKA MALEZI YA WATOTO IKUNGI
Studio Narration JAMBO FM

JAMII YATAKIWA KUWA MAKINI KATIKA MALEZI YA WATOTO IKUNGI

0:00 --:--

Jamii imetakiwa kuwa makini katika malezi ya watoto, kwa kuhakikisha wanapewa malezi bora, uangalizi na maadili yanayowawezesha kukua katika mazingira salama na kujenga mustakabali wao.

Rai hiyo, imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Haika Massawe katika Kata ya Ntuntu, wakati akitoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo kwa jamii.

Amebainisha kuwa ila watoto wakue katika misingi bora na yenye maadili, ni jukumu kwa wazazi kusimamia na kufuatilia mienendo ya kimaadili kwa watoto ikiwa ni pamoja na kuwafunda .

Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri a Wilaya ya Ikungi, Bi. Haika Massawe,

Aidha Bi.Massawe amewahamasisha vijana kujiunga katika vikundi vya kiuchumi ili waweze kunufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri, akieleza kuwa mikopo hiyo ni miongoni mwa fursa zinazolenga kuwawezesha wananchi kuongeza shughuli za uzalishaji na kujikwamua kiuchumi.

Sambamba na hilo, amevitaka vikundi ambavyo tayari vimepatiwa mikopo kuhakikisha vinarudisha fedha hizo kwa wakati na kuzingatia masharti yaliyowekwa, ili kuwawezesha wananchi wengine kupata fursa hiyo na kuendelea kunufaika na mikopo hiyo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.