Skip to main content

JAMBO ATAKA KAMBI YA ASKARI KARIBU NA MAKAZI YA VIJIJI KUTOA MSAADA WA HARAKA UVAMIZI WA WANYAMA PORI

Na Saada Almasi, Meatu - Simiyu.

JAMBO ATAKA KAMBI YA ASKARI KARIBU NA MAKAZI YA VIJIJI KUTOA MSAADA WA HARAKA UVAMIZI WA WANYAMA PORI

Na Saada Almasi, Meatu - Simiyu.

Baada ya matukio mbalimbali ya watu kuvamiwa na Tembo katika maeneo yao, kuvunjiwa nyumba, kuwadhuru na kuchukua vyakula, Mbunge wa Jimbo la Meatu mkoani Simiyu, Salum Khamis Jambo amewataka Askari wa Wanyama pori kuweka kambi karibu na maeneo ya vijiji, ili waweze kufika kwa haraka pale wanapopokea taarifa za uvamizi.

Salum amesema hayo wakati akihutubia wananchi wa Kata ya Kimali iliyopo kijiji cha Paji, mara baada ya kuhutubia wakazi wa Mwangudo, Mwanjoro na Mwamishali, ikiwa ni ziara yake ya shukrani kwa wananchi hao kwa kumchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo Oktoba 2025, ambapo kero aliyokutana nayo ni malalamiko ya wananchi juu ya uvanizi wa Wanyama hao.

Katika ziara hiyo ambayo ameambatana na viongozi wa idara za kiserikali ikiwepo Askari kutoka pori la akiba Maswa, Salum amesema pamoja na jitihada ambazo anazifanya kupambana na wanyama hao bado usumbufu umeendelea kwa wananchi kutokana na wanyama hao kuridhika na vyakula ambavyo wanakula binaadamu kiasi cha kusahau makazi yao

“Kati ya vitu vinavyosumbua akili yangu ni suala la tembo ukilala ukiamka simu za wananchi wakihitaji msaada tembo kavamia,na mbaya zaidi hawa wanyama wameweka makazi katika maeneo yetu wameonja mahindi, michembe, mtama na ladha yake wameipata kiasi cha kusahau maeneo ya porini wanakoishi sasa hawataki kurudi wamekuwa wakitafuta nyumba zenye vyakula na kuvamia,” amesema Salum.

Amesema, ”kwasasa serikali imekuja na mpango wa kuweka uzio wa umeme katika maeneo yote ya hifadhi mpango ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni ni imani yetu utafanya kazi vizuri japokuwa ninawataka askari hawa wafike katika maeneo yetu waweke kambi,"

"Nipo tayari kutoa gharama zote za wao kuishi karibu ndani ya vijjiji na si kukaa Mwanhuzi kwa kuwa bado wapo wanyama ambao wanaishi vijijini hivyo iwe rahisi wanapopata taarifa wawafikie tembo na kuwarudisha porini kusudi isije kutokea uzio unajengwa porini kumbe tembo wamebaki makazi ya watu,” ameongeza Salum.

Kwa upande wake Askari wa Wanyama pori kutoka pori la akiba Maswa, Amideus Makungu amewaambia wananchi hao kuwa, wataanza na zoezi hilo la uwekaji uzio, ambapo pia wataanza kazi wiki hii kuanzia kijiji cha Makao kata ya Mwangudo kuelekea kijiji cha Mbugayabanya  ikiwa ni kilometa 20 na baadaye kufika Damidami wilyani Bariadi

“Zoezi hili linatarajiwa kuanza mapema wiki ijayo na nitoe wito kwa wakazi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano pale ambapo tutafika kufanya shughuli hii katika maeneo yao kwa maana yapo maeneo ambayo yanamilikiwa na wananchi lakini ni mapori ambapo hakuna barabara zinazopitika sasa tembo anapokimbilia kule inakuwa vigumu sana kumpata na kumrudisha hifadhi,” amesema Amideus.

Ziara ya Mbunge wajimbo la Meatu imefanyika katika kata zote 16 za jimbo hilo kwa lengo la kuwashukuru na kufanya ufuatiliaji wa ahadi zake ambazo amezitoa kipindi cha uchaguzi na ambazo hadi hivi sasa tayari kila kata utekelezaji unaendelea kufanyika.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.