Mbunge wa jimbo la Meatu Salum Khamis Salum (Jambo) amedhamiria kumaliza matatizo yanaowakabili wakazi wa jimbo hilo kwa kuhakikisha changamoto ambazo zimwakabili kwa muda mrefu anazitatua kabla ya kipindi cha miaka mitano kumalizika kutokana na hilo katika kipindi chake cha mwaka mmoja ametoa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 580 zikiwa ni fedha zake za mfukoni katika kukabiliana na changamoto hizo.
Moja kati ya changamoto kubwa ambayo imekuwa ikiwatatiza wakazi wa jimbo hilo ni kukosekana kwa huduma ya maji safi na salama na hii ni kutokana na wilaya ya Meatu kuwa na asili ya nusu jangwa hali ambayo inapelekea maji kupatikana kwa tabu hasa kipindi cha kiangazi.
Katika ahadi zake kipindi cha kuomba ridhaa ya kuongoza jimbo hilo Jambo alitoa vipaumbele vyake ikiwa ni pamoja na suala la maji ,kumaliza magofu yote bila kuchangisha wananchi,kupambana na tembo wanaovamia makazi ya watu,kupigania bei ya pamba na kuishawishi serikali kuruhusu wanunuzi zaidi ya mmoja zikiwa ahadi ambazo hadi sasa amezifanikisha kwa kiasi kikubwa.
Hadi hivi sasa katika kata 16 za jimbo hilo kila moja imepokea fedha kwa ajili ya ujenzi ukarabati na umaliziwaji wa miradi iliyosimama kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kujenga shule ya Sekondari Imalaseko ambayo hadi sasa zimetumika zaidi ya milioni 50 kati ya milioni 85 zilizotumika katika kata hiyo ambayo inakwenda kuwa muarobaini kwa wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 ambao walilazimika kwenda mikoa jirani kutafuta elimu hiyo.
Hivi karibuni Jambo akiwa na wajumbe wa Chama cha Mapinduzi kata ya Mwabuzo katika semina kwa wajumbe wa chama hicho semina ambazo zilikuwa zikifanyika nchi nzima amewahakikishia wakazi hao kuwa ndani ya mwaka mmoja wa uongozi wake atahakikisha changamoto zilizokuwa zinawatatiza zimemalizika ama kukaribia kuisha.
“Tumejenga kituo cha polisi tumemaliza,tumekarabati madarasa na nyumba za watumishi ili wazidi kuwatumikia na mengine mengi kwa hapa tu Mwabuzo zaidi ya milioni 44 tayari zimetumika lengo langu nataka ndani ya miaka mitano nikija hapa nisije kuwapa ahadi nataka nikija hapa mniambie mengine mapya kama yatakuwepo ”amesema Mhe Salum Jambo
“Suala la maji limekuwa likitutesa sana na hadi sasa nimeshawaletea jenereta lipelekwe mtoni kufanya kazi ya kuvuta maji ili tupunguz kuhangaika kutafuta maji,na haya yote nafanya kwa kupitia fedha zangu kwa sababu niliwaahidi kuwatumikia”ameongeza Mhe Salum Jambo
Jambo FM imezungumza na baadhi ya wakazi wa Meatu ambao wamekiri kuona jitihada za mbunge wao na kumwomba aongeze nguvu katika kupambania changamoto ya maji wakitaja kuwa huwachukua muda mwingi wa kutafuta maji badala ya kufanya shughuli za kiuchumi.
“Tulitembea hadi kilometa 7 tunafuata mto kupata maji wakati mwingine wanyama wakali mnakutana nao huko tunalazimika kwenda kwa makundi wakati mwigine tunawabeba watoto ,nao wanaacha kwenda shule kwa sababu tukiondoka tunachelewa kurudi ,lakini mbunge wetu tunamshukuru sana anatupumzisha akina mama “Mwalu Davis mkazi wa Mwabuzo
“Kila siku mpya inapoingia lazima uwaze maji,utachelewa kazini kusubiri maji yatoke ukinge tofauti na hapo ununue kwa wale wanaochota mtoni kwenye vile visima wanavyojichimbia kama huna uwezo wa kununua hilo ni tatizo lingine lakini kwa jitihada alizonazo mbunge wetu nina imani kwa kasi aliyonayo suala ka maji linakaribia kubaki historia”amesema Hussein Jumanne mkazi wa Mwanhuzi
Discussion
Reader comments
0 contributions