Mamlaka za Tehran zimeweka bango kubwa katika Uwanja wa Enghelab, likimtishia waziwazi Rais wa Marekani, Donald Trump, hatua inayoashiria kuongezeka kwa kauli kali zinazoungwa mkono na serikali, wakati wa uchaguzi wa katikati ya muhula Marekani na juhudi za kidiplomasia zinazoendelea Mashariki ya Kati.
Bango hilo, linasomeka kwa maandiahi makubwa yanayosema "Tutamuua Trump" likionekana kwa ufadaha juu ya Uwanja wa Enghelab, wenye shughuli nyingi huko Tehran, ambalo lilimuonesha rais wa Marekani akiwa nyuma ya nondo akiwa ameinamisha kichwa.
Bango lingine, limewekwa karibu na hilo, pia likimwonesha Trump pamoja na Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance, mjumbe maalum Steve Witkoff, na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wakiwa na nyuso zenye damu na suti zilizochakaa, dhidi ya mandhari ya bendera zilizochakaa za Israel na Marekani.

Makumi ya watu walikusanyika uwanjani hapo, wakipunga bendera nyekundu na kubeba mabango yaliyosoma: "Kutakuwa na damu" huku wakiitisha kulipiza kisasi cha kiongozi wao mkuu Ayatollah Ali Khamenei, aliyeuawa katika mashambulizi ya Marekani na Israel Februari 28, yaliyochochea vita vya Mashariki ya Kati.
Miundo mipya ya mabango na maonesho ya kuwadhihaki na kuapa kulipiza kisasi dhidi ya Trump na kujivunia ushindi dhidi ya Marekani vitani yamekuwa yakiwekwa mara kwa mara karibu na Tehran.
Katika siku za hivi karibuni, juhudi mpya za kidiplomasia zimekuwa zikiendelea kuileta Tehran na Washington kujadiliana ili kuzuia kuanza upya kwa mapigano ambayo yameenea katika eneo lote na kupandisha bei duniani.
Discussion
Reader comments
0 contributions