Skip to main content

IRAN YATANGAZA 'KIAMA' CHA KISASI KWA MAREKANI

Iran imesema imeweka shabaha nakufanya mashambulizi mfululizo katika kambi za washirika wa marekani ukanda wa mashariki ya kati, kufuatia kile imeita malipizo ya kisasi dhidiya mashambulizi ya Marekani kwa meli zake 5 za mafuta.

IRAN YATANGAZA 'KIAMA' CHA KISASI KWA MAREKANI
Studio Narration JAMBO FM

IRAN YATANGAZA 'KIAMA' CHA KISASI KWA MAREKANI

0:00 --:--

Iran imesema imeweka shabaha nakufanya mashambulizi mfululizo katika kambi za washirika wa marekani ukanda wa mashariki ya kati, kufuatia kile imeita malipizo ya kisasi dhidi
ya mashambulizi ya Marekani kwa meli zake 5 za mafuta.

Jeshi la walinzi wa mapinduzi ya kiislamu ya iran IRGC, limesema limeweka shabaha ya kuripua meli za vita mbili , meli sita za mafuta na meli 10 za mizigo, karibu na mlango wa Bahari wa
Hormuz.

Katika taarifa za mapema, IRGC imetangaza kuripua kwa makombora kambi shirikishi ya Marekani na Jordan ya Al Azraq nchini Jordan kutokana na kile ilichoeleza kufuatia
mashambalizi ya marekani ya meli 5 za mafuta za iran katika huba ya Oman kando na kisiwa cha Kharg.

Kufuatia hilo Jeshi la Jordan limethibitisha kushambuliwa na Iran likisema limefanikiwa kudungua makombora ya ballistic yapatayo 18 ya iran, yaliyolenga nyumba za makazi huku 2
yakidondoka katika maneo salama bila kuathiri wakazi wa maeneo ya Muwaffaq, Salti na Zarqa.

Mfululizo wa mashambulizi baina ya pande hizo zinazohasimiana, unakuja kufuatia mvutano mkali wa taklibani miezi 6 ya vita vya Marekani, Israel dhidi ya Iran, ulioibuka baada ya kifo cha Kiongozi Mkuu wa Iran Februari 28, 2026, vita vilivyopelekea pia kufungwa kwa mlango bahari wa hormuz na mzingiro uliotangazwa na Marekani katika eneo hilo nyeti.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.