Skip to main content

INEC YAWAFUNDA MAKARANI WA UCHAGUZI MDOGO KAHAMA

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

INEC YAWAFUNDA MAKARANI WA UCHAGUZI MDOGO KAHAMA

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

Makarani waongozaji wa uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Zongomela wametakiwa kusoma Katiba sheria na miongozo ya tume ya uchaguzi Pamoja na kujiepusha kuwa vyanzo vya malalamiko kutoka katika vyama vya siasa.

Wito huo umetolewa na msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Kahama mjini Steven Magala wakati wa ufunguzi  wa mafunzo  hayo kwa makarani 41 ambao watasimamia uchaguzi huo.

“Niwaase sana ndugu zangu makarani waongozaji msiache kusoma Katiba kanuni na maelekezo ya tume ya uchaguzi mnaenda kusimamia uchaguzi basi nendeni mkatende haki na msiwe chanzo cha migogoro baina ya vyama vya siasa” Amesema Magala.

Katika hatua nyingine Magala amesisitiza kutoa kipaumbele kwa watu wenye mahitaji maalum wakiwemo wazee,walemavu na wanawake wajawazito na wenye watoto ili kuwapa nafasi ya kupiga kura na kuendelea na shughuli zao.

“Tunatambua kuwa wapo wapiga kura wana mahitaji maaulumu wakiwemo wazee na wanawake wenye watoto wachanga,wahini vituoni na mtoe nafasi kwa makundi haya wapige kura mapema ili waendelee na majukumu yao” Amesisitiza Magala.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa watayatumia vyema mafunzo waliyoyapata kufanikisha uchaguzi huo na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kikatiba.

“Tutaenda kuyatumia vizuri mafunzo tuliyopata na kuhakikisha tunaenda kusimia uchaguzi kwa haki kwa kufuata maelekezo ya Tume ya uchaguzi,tuombe sana wananchi wajitokeze kupiga kura ili kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua kiongozi ambaye atawaletea maendeleo.” Wamesema washiriki hao.

Uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya  Zongomela utafanyika June Mosi mwaka huu kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo ambaye ni Meya mstaafu wa manispaa ya Kahama Ramdhani Bundala maarufu kwa jina la Ng’wana Ibengwe.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.