Skip to main content

IKUNGI WAIEPUKA ADHA YA MAJI WAKIPATA TABASAMU JIPYA

Na Saulo Stephen-Singida.

IKUNGI WAIEPUKA ADHA YA MAJI WAKIPATA TABASAMU JIPYA

Na Saulo Stephen-Singida.

Mradi wa maji wenye thamani ya Sh. milioni 819.836 uliojengwa kati ya vijiji vya Ikungi na Mbwanjiki, wilayani Ikungi mkoani Singida, umeondoa adha ya ukosefu wa maji safi na salama kwa wananchi 5,095, huku ukiwaepusha na hatari ya kushambuliwa na fisi walipokuwa wakifuata maji nyakati za usiku.

Mradi huo, uliojengwa na Serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa Maji na kutekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), umezinduliwa na Mwenge wa Uhuru 2026.

Mradi unahusisha kisima chenye kina cha mita 125 kinachozalisha lita 20,000 za maji kwa saa, uwezo unaotarajiwa kuhakikisha wananchi wa eneo hilo wanapata huduma endelevu ya maji safi na salama.

Akitoa taarifa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Mwang'onda, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Ikungi, Mhandisi Shafii Shabani, alisema mradi huo umeleta mageuzi makubwa katika upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi.

Alisema pamoja na kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama, mradi huo umechangia kupunguza magonjwa yanayotokana na matumizi ya maji yasiyo salama, kuboresha usafi wa mazingira na kuinua ustawi wa jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Mwang'onda, alisema Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza kwa vitendo dhamira yake ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu za kijamii, ikiwemo maji safi na salama.

Alisema uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali katika miradi ya maji umeendelea kuwaondolea wanawake adha ya kutembea umbali mrefu na kubeba ndoo kichwani kutafuta maji, hatua inayochochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika maeneo mbalimbali nchini.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.