Skip to main content

IFAHAMU TRENI NDEFU ZAIDI AFRIKA KATIKA REKODI YA DUNIA

Kwa mara ya kwanza Africa inaingi katika rekodi ya dunia ya kuwa na Treni ya Mizigo Ndefu Zaidi yenye Urefu wa Kilomita 7.6

IFAHAMU TRENI NDEFU ZAIDI AFRIKA KATIKA REKODI YA DUNIA
Studio Narration JAMBO FM

IFAHAMU TRENI NDEFU ZAIDI AFRIKA KATIKA REKODI YA DUNIA

0:00 --:--

Kwa mara ya kwanza Africa inaingi katika rekodi ya dunia ya kuwa na Treni ya Mizigo Ndefu Zaidi yenye Urefu wa Kilomita 7.6

Nchi ya Afrika Kusini iliyoko kusini mwa Bara la Africa imeweka rekodi mpya ya dunia baada ya kuendesha treni ya mizigo yenye urefu wa kushangaza wa kilomita 7.6 (sawa na maili 4.7).

Urefu huo kwa mchanganuo wa urefu kwenda juu ni sawasawa na urefu wa jengo lenye ghorofa 2,530, hivyo kwa rekodi ya jengo refu ulimwenguni la Burj Khalifa la Dubai lenye jumla ya ghorofa 163 yakusanyike yawe 9, huku umbali wa barabara kwa miji ya Tanzania ni sawa na kutoka katikati ya Jiji la Dar es salaam Posta hadi Kinondoni.

Shirika la usafirishaji la serikali nchini Afrika kusini, Transnet limetangaza kuwa treni hiyo ambayo ilikuwa imeunganishwa na mabehewa 696 imekamilisha safari yake ya majaribio mnamo Oktoba 18 ya mwaka huu.

Treni hiyo ndefu ilisafiri umbali wa kilomita 860, ikianzia katika Bandari ya Saldanha Bay iliyopo pwani ya magharibi hadi katika migodi ya madini ya chuma iliyopo ndani ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa mchanganuo wa kisayansi Ili kufanikisha usafiri wa msafara huo mkubwa bila kukwama ni lazima injini za umeme na dizeli ziwekwa katika sehemu mbalimbali katikati na pembezoni mwa mstari wa mabehewa ili kutoa nishati ya kutosha ya kusukuma na kuvuta.

Duru kutoka Africa ya kusini zimeripoti kuwa wakati ya safari ya majaribio mabehewa yote 696 yalikuwa matupu bila mzigo

Kwa mujibu wa takwimu za usafiri wa treni ulimwenguni zinaeleza kuwa kawaida, treni za mizigo kote duniani huwa fupi zaidi, mara nyingi zikiwa na urefu wa kati ya maili nusu (km 0.8) hadi maili moja na nusu (km 2.4).

Hata hivyo Shirika la Transnet limesema jaribio hili limevunja rekodi ya awali iliyowekwa nchini Australia mwaka 2001, ambapo treni ya mizigo yenye urefu wa maili 4.5 sawa na kilomita 7.2 ilisafiri kati ya mgodi wa chuma na bandari moja huko Magharibi mwa Australia.

Kufuatia rekodi hii iliyowekwa na Africa kusini, sasa Africa kusini inakuwa kileleni katika rekodi zilizowahi kushikwa ulimwenguni kuwa na treni ndefu ikitupa chini rekodi ya Australia Treni ya kampuni ya BHP nchini Australia.

Hiyo ilifikisha urefu wa kilomita 7.35 (maili 4.5) ikiwa na mabehewa 682 ya madini ya chuma na injini 8, Marekani Treni ndefu zaidi za makontena (intermodal container trains) iliyofikia hadi urefu wa kilomita 6.1.

India treni ya majaribio iliyopewa jina la Super Vasuki yenye urefu wa kilomita 3.5, Mauritania & Brazil Treni za kibiashara zinazobeba madini ya chuma na nafaka zenye urefu wa takriban kilomita 3.0.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.