Skip to main content

IBINDI YOUTH VISION DAY YAFANA KATAVI, MDAKUNI AAHIDI 'KUIPIGA TAFU'

Na Daniel Gahu - Katavi.

IBINDI YOUTH VISION DAY YAFANA KATAVI, MDAKUNI AAHIDI 'KUIPIGA TAFU'

Na Daniel Gahu - Katavi.

Katika hatua ya kuunga mkono maendeleo ya vijana na kukuza sekta ya sanaa, Diwani wa Kata ya Ibindi, iliyopo halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi, Mdakuni Ramadhani Matongo, ameahidi kukinunulia kikundi cha sanaa cha Ibindi Youth Vision kamera pamoja na vifaa vya kisasa vya uzalishaji wa maudhui.

Ahadi hiyo ameitoa Julai 27, wakati akizungumza katika hafla ya Ibindi Youth Vision Day iliyofanyika katika Ukumbi wa Logaa, uliopo Kata ya Ibindi, mbele ya viongozi mbalimbali, wanachama wa kikundi hicho na wananchi waliojitokeza kushiriki maadhimisho hayo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Diwani Matongo amesema kuwa uwekezaji katika vifaa vya kisasa vya kazi, utawapa vijana uwezo wa kuzalisha kazi zenye ubora wa hali ya juu, kuongeza ushindani wao katika soko la sanaa na maudhui ya kidijitali, pamoja na kuwafungulia fursa mpya za ajira na kujiajiri.

Ameeleza kuwa serikali na viongozi wa jamii wana wajibu wa kuendelea kuwekeza katika maendeleo ya vijana kwa kuwa wao ndiyo nguvu kazi ya taifa na nguzo muhimu katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

"Tunataka kuona vijana wa Ibindi wanatumia vipaji vyao kujiletea maendeleo na kuitangaza kata yetu. Hivyo, tutahakikisha wanapata vifaa vinavyowawezesha kufanya kazi zao kwa weledi na ubora unaokidhi ushindani wa sasa," amesema Matongo.

Mbali na ahadi hiyo, Diwani huyo amewataka vijana kuendelea kushirikiana kwa umoja, kutumia vyema fursa zinazojitokeza katika sekta ya sanaa na teknolojia, pamoja na kufanya kazi kwa bidii, nidhamu na ubunifu ili kufikia malengo yao.

Kwa upande wao, wanachama wa kikundi cha Ibindi Youth Vision wameeleza kufurahishwa na ahadi hiyo wakisema kuwa upatikanaji wa kamera na vifaa vya kisasa utakuwa chachu ya kuboresha kazi zao, kuongeza ubora wa uzalishaji wa maudhui na kuwafikia watazamaji wengi zaidi.

Hatua hiyo inatajwa kuwa sehemu ya jitihada za kuimarisha vipaji vya vijana na kukuza uchumi kupitia sekta ya sanaa, ambayo imeendelea kuwa chanzo muhimu cha ajira na kipato kwa vijana wengi nchini.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.