Skip to main content

HUDUMA BORA ZA AFYA KUWANUFAISHA WANANCHI 5,984 SINGIDA

Na Saulo Stephen - Singida.

HUDUMA BORA ZA AFYA KUWANUFAISHA WANANCHI 5,984 SINGIDA
Studio Narration JAMBO FM

HUDUMA BORA ZA AFYA KUWANUFAISHA WANANCHI 5,984 SINGIDA

0:00 --:--

Na Saulo Stephen - Singida. 

Wananchi wapatao 5,984 wa Kata ya Unyamikumbi katika Manispaa ya Singida wanatarajiwa kunufaika na huduma bora za afya kupitia mradi wa ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika Zahanati ya Unyamikumbi unaotekelezwa kwa gharama ya jumla ya Shilingi milioni 148.5 hadi kukamilika kwake.

Akizungumza kuhusu maendeleo ya mradi huo, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Unyamikumbi, Nuhu Fute, amesema utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 70, ambapo hadi sasa kiasi cha Shilingi milioni 79.08 tayari kimetumika katika shughuli mbalimbali za ujenzi.

Amesema kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia kuboresha kwa kiwango kikubwa huduma za afya ya mama na mtoto, kupunguza msongamano wa wagonjwa katika vituo vingine vya afya pamoja na kuongeza upatikanaji wa huduma za msingi kwa wananchi wa Unyamikumbi na maeneo ya jirani.

Jengo hilo la kisasa lilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi katika hatua za awali, huku Serikali ikiendelea na kazi za umaliziaji kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Singida.

Serikali imeendelea kusisitiza dhamira yake ya kuwekeza katika miradi ya maendeleo ya kijamii hususan sekta ya afya, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi kwa wakati na kwa ubora unaostahili.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.