Skip to main content

HOFU YA EL-NINO: MTO LAMADI WAPANDISHA HOMA KWA WANANCHI BUSEGA

Na Saada Almasi, Lamadi - Simiyu.

HOFU YA EL-NINO: MTO LAMADI WAPANDISHA HOMA KWA WANANCHI BUSEGA

Na Saada Almasi, Lamadi - Simiyu.

Kufuatia tahadhari zilizotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), juu ya mvua kubwa zinazotarajiwa kuanzia wiki za mwisho wa Septemba, 2026, wananchi wa Kata ya Lamadi wilaya ya Busega mkoani Simiyu wamejaa hofu kutokana na mto Lamadi ambao umekuwa ukiwasababishia mafuriko kila kipindi cha msimu wa mvua.

Mto huo, kwasasa umejaa magugu maji ambayo yanatokea katika Hifadhi ya wanyama ya Serengeti na umekatiza karibu na makazi ya wananchi kuelekea katika Ziwa Viktoria ambapo humwaga mwaji yake unazidi kuwatia hofu kutokana na kutokuwa na dalili za kupungua maji yake.

Diwani wa Kata ya Lamadi Joseph Goryo amekiambia kituo hiki kwamba kwa sasa mto huo tayari umejaa maji kiasi cha kufika maeneo ya makazi huku changamoto kubwa inayoonekana ni magugu maji ambayo yameziba njia za kutokea maji na kusababisha kasi ya maji kutoka kuelekea ziwani kuwa mdogo.

“Huu mto umepokea magugu maji mengi kutokea mbuga ya Serengeti na yamezingira eneo kubwa la mto kiasi cha kuziba njia za maji kupita sasa ukiendelea hivi na mvua zinazokuja hatari itakuwa kubwa sana,tayari kipindi cha mvua za kawaida watu walikuwa wanaathirika kwa mafuriko ya mto huu sasa hizo mvua kubwa itakuwaje ndiyo maana watu wamejaa hofu,” alisema Joseph Goryo, Diwani wa kata ya Lamadi.

Amesema, “tayari tumefanya mawasiliano ya Wakala wa Barabara  Mijini na Vijijini (TARURA ) watusaidie kufanya maboresho ya njia za kupitishia maji hasa katika mitaro yote iliyoziba waizibue ili maji yapite katika mkondo wake yasiingie katika makazi,pia tumewaomba wananchi ambao wapo katika mabonde waanze kuja juu watafute makazi mapya kama tahadhari ya kuokoa maisha yao.”

Mwalu Deus mfanyabiashara na mkazi wa kitongoji cha Kisesa wilayani humo ambaye msimu wa mvua uliopita aliathirika baada ya kuvamiwa na mafuriko na kuharibu biashara zake anaiomba serikali kuwasaidia kuondoa magugu hayo ili yale waliyopitia msimu uliopita yasijirudie.

“Mimi na wenzangu tumekuwa wafanyabiashara wa matunda kwa muda mrefu hapa Kisesa,msimu uliopita maji ya huu mto yalifika huku kwetu na biashara zikaharibika tukapata hasara,kwa hiyo tunaiomba serikali itusaidie isafishe njia ili haya maji yakija yaweze kwenda moja kwa moja ziwani kusiwepo na vizuizi,tunaogopa kwa kweli”amesema Mwalu

Hata hivyo, tayari uongozi wa kata hivyo umekubaliana kutenga maeneo ya shule kama tahadhari ya kuhifadhi watu ambao makazi yao yataathirika na mafuriko endapo yatatokea na kuwakosesha makazi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.