Tumekuwa tukishuhudia picha za video kutoka pembe mbalimbali duniani zkionesha wakati wa kutisha ndege binafsi ya Learjet ilipoanguka.
Pia kuna rekodi za sauti zinazodaiwa kunasa dakika za mwisho ndani ya ndege, ambapo inaonekana hofu kubwa katika sauti ya rubani akitoa taarifa ya safari na kuomba msaada.
FIKRA.
Ni vigumu kufikiria hofu ambayo watu hao tisa walipitia ndege ilipokuwa ikishuka kwa kasi kuelekea ardhini, ikiwa inaonekana hakuna njia ya kuzuia kilichokuwa kinatokea.

Taarifa za safari ya ndege zinaripoti kuwa Learjet iliingia katika mteremko mkali sana, kwa wakati mmoja ikizidi futi 30,000 kwa dakika. Ndege iligonga ardhi kwa nguvu kubwa kiasi kwamba ilipasuka na kuwa vipande maelfu.
ATHARI.
Ndege ya tani nyingi inapogonga ardhi kwa kasi na pembe kali kiasi hicho, athari inaweza kuwa ya uharibifu mkubwa. Nguvu kubwa ya kasi inaweza kusababisha ndege kukandamizwa vikali, kuvunjika vipande vipande na sehemu za mabaki yake kuzama ardhini.
Hii ndiyo inayoelezea kwa nini baadhi ya ajali za ndege zenye mgongano mkali huacha nyuma kile kinachoonekana kama shimo kubwa badala ya ndege inayotambulika.
Matenki ya mafuta yanaweza kupasuka, moto unaweza kuwaka, na joto linalotokana na moto linaweza kuharibu zaidi mabaki ya ndege.
Vipuri vya ndege vinaweza kukandamizwa, kuteketea, kuzikwa au kutawanyika katika eneo lote la ajali.

UTAMBUZI.
Kutokuwepo kwa ndege inayotambulika haimaanishi kuwa hapakuwa na ndege, inaweza kumaanisha kuwa mgongano ulikuwa na nguvu kiasi kwamba ni kidogo sana kilichobaki kikiwa kizima.
Zaidi ya maelezo ya kiufundi, kuna simulizi ya kibinadamu ya kusikitisha sana hapa, fikiria kuwa ndani ya ndege hiyo, ukitambua kuwa inaanguka kwa kasi kuelekea ardhini na ukijua kuwa unaweza usiwe na udhibiti wowote wa kile kitakachotokea baadaye.
UTU.
Tuwakumbuke familia na wapendwa wa wale waliopoteza maisha, kwani wanapitia maumivu yasiyofikirika, ili tu kukutana na uvumi wa mitandaoni kutoka kwa watu wanaodai kuwa ndege haikuwepo kabisa kwa sababu tu hawawezi kutambua mabaki yake.

Tuoneshe heshima na huruma. Hawa waliokuwa watu halisi, na familia zao zinastahili utu wakati wanaomboleza wapendwa wao.
KUHUSU AJALI:
Chanzo rasmi cha ajali ya ndege iliyoua watu tisa Florida bado hakijatolewa, lakini Mamlaka za usafiri wa anga nchini Marekani zimesema uchunguzi unaendelea.
Kwa mujibu wa taarifa ya awali kutoka Bodi ya Kitaifa ya Usalama wa Usafiri (NTSB) na Shirika la Usafiri wa Anga (FAA), ndege aina ya Learjet 60 yenye namba ya usajili N722BD ilikuwa katika urefu wa futi 35,000 ikitoka Austin, Texas kuelekea Bahamas.
Mawasiliano ya mwisho kati ya rubani na kituo cha kudhibiti anga (ATC) yanaonesha rubani aliripoti changamoto kadhaa. Alidai kuna barafu iliyokuwa inaganda kwenye ndege (icing), mtikisiko wa wastani (turbulence) pamoja na mvua kubwa.

Baada ya taarifa hiyo, hali ilibadilika ghafla. Ndege ilianza kushuka kwa kasi ya ajabu. Data za safari zinaonesha iliporomoka kwa futi takriban 27,000 ndani ya dakika moja tu, huku taarifa nyingine zikieleza kushuka kwa futi hadi 32,000 kwa dakika.
Katika muda huo, rubani alitangaza dharura (Mayday) na kuripoti tatizo la overspeed, maana yake ndege ilizidi mwendo wa juu unaoruhusiwa wa Mach 0.81 hadi karibu Mach 0.90, na kudunda kwa pua karibu wima.

Rubani Msaidizi, Nathalia Filgueiras (20) - RIP.
Mpaka sasa sababu halisi ya kuanguka bado ni nadharia. Wataalamu wa anga wanaangalia uwezekano wa mambo matatu makuu.
Kwanza ni athari ya barafu kwenye tailplane, ambapo barafu inaweza kusababisha tailplane stall na kuifanya pua ya ndege kudunda ghafla bila rubani kuweza kuirudisha.
Pili ni hali iitwayo Mach tuck, ambapo kwa mwendo mkubwa sana mawimbi ya hewa kwenye mabawa husababisha ndege kudunda yenyewe na nguvu za upepo kuibamiza.

Tatu ni hali ya hewa. Ilielezwa kuwa kulikuwa na dhoruba kali Florida siku hiyo, ingawa FAA bado haijaunganisha moja kwa moja hali ya hewa na ajali.
Na ndiyo maana wakati ndege hiyo ilipogonga eneo la Military Trail na 10th Avenue North karibu na Greenacres, iliacha shimo kubwa barabarani na kulipua bomba la maji, na kusababisha watu takriban 600 kuhamishwa kwenye makazi ya jirani.
Discussion
Reader comments
0 contributions