Uchapakazi, weledi na heshima ya Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan katika uongozi, ilianza kuonekana mapema tangu alipokuwa Makamu wa Rais, kama ilivyowahi kusimuliwa na mtangulizi wake, hayati Dkt John Magufuli.
Dkt Magufuli, ambaye leo inaadhimishwa miaka mitano tangu kifo chake, Machi 17, 2021 alilithibitisha hilo, mbele ya Mkutano Mkuu wa CCM, uliofanyika mwaka 2020, aliposema Dkt Samia ni mchapakazi na mwenye heshima.
Katika maelezo yake, alisema Dkt Samia ni mchapakazi na mwenye heshima na kwamba kila alipomtuma alikwenda kufanya kazi kama ilivyopaswa.

Discussion
Reader comments
0 contributions