Na Eunice Kanumba –Shinyanga.
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) mkoani Shinyanga, imebaini kuwepo kwa uharibifu wa taa za barabarani 400 zenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 839.2 hali ambayo imedaiwa kuleta hasara.
Hayo yameelezwa na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Ntuli Mwaikokesya wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya malalamiko ya wananchi kuhusu kutokuwepo kwa baadhi ya taa kwenye barabara huku akieleza uwekaji wa taa mpya moja gharama yake ni shilingi Milioni 3.5 hadi Milioni 4.
Amesema, taa zilizo haribika ni 400 zenye thamani ya zaidi ya shilingi Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Ntuli Mwaikokesya 839.2 ambapo baada ya kubaini walianza ukarabati wa taa 259 uliogharimu zaidi ya shilingi Milioni 543.4.

Mhandisi Mwaikokesya ameeleza kuwa barabara ya Manonga Nyasamba kuna taa 184 zenye thamani ya shilingi Milioni 386.02 ambazo zimerekebishwa ni taa 85 kwa zaidi ya shilingi milioni 178.3 huku Shinyanga – Bubiki kuna taa 75 za shilingi Milioni 157.3 ambazo hazijakarabatiwa ni taa 56 zenye thamani ya shilingi 117.4
“Katika ukarabati huo bado taa 114 zinatakiwa kurekebishwa kwa zaidi ya shilingi Milioni 295.8 ambapo hatua zinazochukuliwa ni kuongea na viongozi wa maeneo husika ili kuhamasisha ulinzi shirikishi,” alisema Mhandisi Mwaikokesya.
Mwaikokesya amesema maeneo ambayo hayajarekebishwa taa fedha zikipatikana watajitahidi kuhakikisha marekebisho yanafanyika kwa haraka.

Ameongeza kuwa, kila mwananchi anatakiwa kuwa mlinzi kwani serikali inawekeza fedha nyingi na wanaofanya uhalibifu wako ndani ya familia na jamii inayozunguka.
“Serikali ina majukumu mengi kuhakikisha inaleta maendeleo lakini miundombinu isipolindwa tutakuwa hatutendea haki fedha zinazoletwa sababu tutakuwa kama tunakarabati mradi mmoja na maendeleo kuchelewa nakubaki kulalamika,” amesema Mhandisi Mwaikokesya.
Discussion
Reader comments
0 contributions