Macho ya Watanzania na Wakenya yanaelekezwa jijini Mwanza, ambako Charlene Ruto, binti wa Rais wa Kenya, William Ruto, anatarajiwa kufunga ndoa na mchumba wake Mtanzania, Isaya Yunge, kesho Novemba 6, 2026.
Ndoa hiyo inatarajiwa kufungwa katika eneo la ufukwe wa Hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza, huku maandalizi ya sherehe hiyo yakivuta hisia za watu kutoka mataifa hayo mawili.

Picha za ‘Pre-Wedding’ za wawili hao zimeanza kuvutia hisia za watu mitandaoni, zikionesha mandhari na namna wanavyojiandaa kuanza ukurasa mpya wa maisha yao ya ndoa.
Tukio hilo linatarajiwa kukutanisha ndugu, jamaa na wageni mbalimbali kutoka Tanzania na Kenya, huku Mwanza ikitarajiwa kuwa kitovu cha shamrashamra za muungano huo wa kifamilia.



Discussion
Reader comments
0 contributions