Skip to main content

HALMASHAURI ZATAKIWA KUANDAA MIPANGO GHARAMA ZA UDHIBITI TAKANGUMU

Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), imezikumbusha Halmashauri kutekeleza agizo la Waziri wa nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, la kuandaa mipango ya udhibiti wa takangumu inayoainisha hatua za utekelezaji, gharama na vyanzo vya fedha, ili kuimarisha usafi wa mazingira katika miji na vijiji.

HALMASHAURI ZATAKIWA KUANDAA MIPANGO GHARAMA ZA UDHIBITI TAKANGUMU
Studio Narration JAMBO FM

HALMASHAURI ZATAKIWA KUANDAA MIPANGO GHARAMA ZA UDHIBITI TAK...

0:00 --:--

Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), imezikumbusha Halmashauri kutekeleza agizo la Waziri wa nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, la kuandaa mipango ya udhibiti wa takangumu inayoainisha hatua za utekelezaji, gharama na vyanzo vya fedha, ili kuimarisha usafi wa mazingira katika miji na vijiji.

Akizungumza wakati wa kufunga kikao kazi cha siku mbili kuhusu usafi wa mazingira na udhibiti wa takangumu katika ukumbi wa VETA jijini Dodoma, Mratibu wa Huduma za Afya na Usafi wa Mazingira kutoka OWM-TAMISEMI, Selemani Yondu amesema, Halmashauri zinapaswa kuandaa mipango hiyo ndani ya wiki mbili kama ilivyoelekezwa, kwa kuzingatia shughuli za muda mfupi, wa kati na mrefu.

“Tunataka mpango unaoonesha shughuli zitakazotekelezwa, gharama zake na fedha zitatoka wapi. Vyanzo hivyo vinaweza kujumuisha bajeti za Halmashauri na Serikali Kuu, ada za taka, uwekezaji na michango ya wadau. Tutaandaa kielelezo cha pamoja ili iwe rahisi kuunganisha na kuchambua mipango ya Halmashauri,” amesema Yondu.

Aidha, amewataka maafisa wa Halmashauri kuwasilisha taarifa zinazohitajika kwa wakati na kutekeleza majukumu yao kwa uwajibikaji. Aidha, awapongeza Amepongeza zinazochukua hatua zinazochukuliwa na Halmashauri nchini katika kuhakikisha Usafi unafanyika na taka zinaondoshwa maeneo yao na kuwaomba kuendeleza jitihada hizo ili kuiweka Miji katika hali ya Usafi.

Kwa upande wake, Mratibu wa Udhibiti wa Takangumu kutoka Wizara ya Afya, Evance Simkoko amesema, wizara hiyo itaendelea kushirikiana na OWM-TAMISEMI, Mikoa na Halmashauri katika kukabiliana na changamoto za usafi wa mazingira.

Amesema ushirikiano kati ya maafisa afya, wakuu wa vitengo na viongozi wa ngazi mbalimbali utasaidia kuimarisha udhibiti wa taka na kulinda afya za wananchi.

Simkoko amewapongeza washiriki kwa michango yao katika kikao hicho, akisema maoni waliyotoa yataisaidia timu ya uratibu kuboresha utekelezaji wa shughuli za usafi wa mazingira. Amewahimiza wataalamu kuomba ufafanuzi pale maelekezo yanapokuwa hayajaeleweka ili kazi zifanyike kwa wakati.

Naye Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Mji Kondoa, Alfred Chakalike amesema, atawashirikisha wenzake maarifa aliyoyapata katika kikao hicho kwani yatasaidia kuboresha ukaguzi wa usafi wa mazingira na elimu kwa wananchi kuhusu kuhifadhi taka katika vyombo maalumu.

Kikao kazi hicho kimewahusisha wataalamu kutoka OWM-TAMISEMI, maafisa afya wa Mikoa na Halmashauri, pamoja na wakuu wa vitengo vya udhibiti wa taka.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.