Skip to main content

HALI TETE SUDAN: VITA, UKAME VYAONGEZA BALAA LA NJAA

Zaidi ya watu 135,000 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na vita vinavyoendelea nchini Sudan.

HALI TETE SUDAN: VITA, UKAME VYAONGEZA BALAA LA NJAA
Studio Narration JAMBO FM

HALI TETE SUDAN: VITA, UKAME VYAONGEZA BALAA LA NJAA

0:00 --:--

Zaidi ya watu 135,000 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na vita vinavyoendelea nchini Sudan.

Kwa mujibu wa mfumo wa Kimataifa wa Kupima Viwango vya Uhaba wa Chakula (IPC) umetoa onyo kali kuwa migogoro ya silaha pamoja na ukame mkali vinaendelea kuzorotesha usalama wa chakula katika maeneo ya Taifa la Sudan hasa Darfur na Kordofan.

Kwa mujibu wa takwimu hizo pia ukame mkali unaohusishwa na mfumo wa hali ya hewa wa El Niño umeathiri zaidi ya nusu ya eneo la Sudan, hatua iliyosababisha kushindwa kustawi kwa mazao na kupekelekea kukosa vyanzo vya chakula na kipato kwa familia kubwa za nchi hiyo.

Takwimu hizo zinaeleza hadi Kufikia mwezi Mei, karibu watu milioni 19.5 (zaidi ya 40% ya wananchi wote) wa Taifa hilo walikuwa wakikabiliwa na viwango vya juu vya uhaba mkali wa chakula, huku Zaidi ya watu 135,000 wako katika Awamu ya 5 ya IPC kiwango kinachotajwa kuwa cha juu zaidi cha janga la njaa kutokana na ukosefu mkubwa wa chakula, utapiamlo uliokithiri, na vifo vinavyotokana na magonjwa au njaa.

Takwimu hizo zinaelezwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na Vita vilivyoanza Aprili 2023 kati ya Jeshi la Serikali na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) ambavyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 150,000 (kwa mujibu wa shirika la ACLED) na kuwafanya watu karibu milioni 13 kukimbia makazi yao wenyewe.

"Bila kuwa na ongezeko la haraka na kubwa la msaada wa kibinadamu nchini Sudan, ukosefu wa chakula, utapiamlo mkali, na vifo vya ziada vitaongezeka kwa kasi." Afisa wa ACLED.

Duru kutoka nchini Sudana zinaarifu kwamba tukio la hivi karibuni la vurugu, shambulio la angani limewaua zaidi ya raia 72 wachimbaji wadogo wa dhahabu katika eneo la mpakani kati ya Sudan na Misri.

Kundi la wanasheria wa kutetea haki za binadamu nchini Sudan (Emergency Lawyers) lilidai kuwa ndege za vita za Misri ndizo zilizowalenga wachimbaji hao.

Hata hivyo, Jeshi la Misri lilitoa taarifa likieleza kuwa limeanzisha operesheni kubwa ya kupambana na uchimbaji haramu wa madini katika Jangwa la Mashariki kwa kurusha "vipeperushi vya onyo" kwa wananchi, bila kutoa maelezo zaidi.

Vuguvugu la mapigano kati ya Jeshi la Serikali ya Sudan (SAF - Sudanese Armed Forces) Linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan dhidi ya vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF - Rapid Support Forces) vinavyoongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo maarufu “Hemedti’, liliibuka baada ya kutokea kwa mvutano na utofauti wa kimtazamo kati ya viongozi hao kuhusu mpango wa kuliingiza kundi la RSF ndani ya jeshi la taifa (SAF) na nani kuwa amiri jeshi mkuu wakati wa kipindi cha ushirikiano wa kuelekea utawala wa kiraia.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.