Skip to main content

HALI NI MBAYA DRC: VISA VIPYA VYA EBOLA 9000, VIFO 4000

Rekodi Mbaya Zaidi ya mlipuko wa virusi vya Ebola imeripotiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

HALI NI MBAYA DRC: VISA VIPYA VYA EBOLA 9000, VIFO 4000
Studio Narration JAMBO FM

HALI NI MBAYA DRC: VISA VIPYA VYA EBOLA 9000, VIFO 4000

0:00 --:--

Rekodi Mbaya Zaidi ya mlipuko wa virusi vya Ebola imeripotiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mamlaka za afya Nchini Congo zimeeleza kuwa mlipuko wa ugonjwa huo umeongezeka kasi zaidi nakufikia visa 9,000 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 4,000.

Idadi hiyo inakuwa ni kubwa zaidi tangu mlipuko wa ugonjwa huo ulipotangazwa mapema mwezi mei 2026

Walakini wataalamu wa afya wanaeleza kuwa virusi hivyo vilianza kusambaa wiki kadhaa au hata miezi kabla ya kubainika

Huu unakuwa ni mlipuko wa 17 wa Ebola nchini Congo wakwanza ukibainika mnamo Agosti mwaka 1976, ambapo ulianzia kwa kasi ya kuchipukia katika Mkoa wa Ituri kaskazini mashariki mwa DRC na kusambaa katika mikoa saba ya kaskazini na mashariki mwa nchi hiyo.

 Kwa mujibu wa takwimu za kisayansi mlipuko wa sasa unasababishwa na virusi aina ya Bundibugyo (Bundibugyo strain), ambacho hadi sasa hakina chanjo wala matibabu rasmi yaliyoidhinishwa.

Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza siku ya Jumanne kuwa jaribio la kliniki (clinical trial) la chanjo mpya dhidi ya virusi hivyo limepangwa kuzinduliwa nchini DRC ndani ya mwezi huu wa Oct.

Mpaka sasa virus ivya Ebola vimeripotiwa kusambaa kwa zaidi ya nchi 6 ulimwenguni zikiwemo Uholanzi, Ujerumani, na Ufaransa kwa nje na Congo, Uganda na Kenya kwa ndani ya Africa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.