Skip to main content

HAKUNA CHANGAMOTO YA HUDUMA ZA USAFIRI SINGIDA - LATRA

Na Saulo Stephen - Singida.

HAKUNA CHANGAMOTO YA HUDUMA ZA USAFIRI SINGIDA - LATRA

Na Saulo Stephen - Singida.

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Mkoa wa Singida, imesema hadi sasa hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza katika huduma za usafiri wa abiria kutokana na ongezeko la bei ya mafuta.

Hayo yamesemwa na Afisa Mfawidhi wa (LATRA) Mkoa wa Singida, Anord Selwana wakati akiongea na Jambo Media Ofisini kwake, amesema hali hiyo imechangiwa na ushirikiano mzuri kati ya LATRA, wamiliki wa vyombo vya usafiri pamoja na mawakala, baada ya kukutana na kukubaliana kufuata maelekezo ya Serikali kuhusu marekebisho ya nauli.

Afisa Mfawidhi wa (LATRA) Mkoa wa Singida, Anord Selwana.

Amebainisha kuwa hadi sasa hakuna malalamiko yoyote yaliyopokelewa kutoka kwa wananchi wanaotumia huduma za usafiri mkoani humo.

Aidha akizungumzia kuhusu bajaji, Selwana amefafanua kuwa LATRA haina mamlaka ya kupanga nauli za vyombo hivyo kwa kuwa vinahesabika kama usafiri wa kukodi, sawa na mabasi ya kifahari (luxury bus), huku akitoa wito kwa wamiliki wa bajaji na vyombo vingine vya usafiri kuendelea kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na LATRA, ili kuhakikisha huduma bora na salama kwa wananchi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.