Skip to main content

GGML MGUU SAWA USHIRIKI DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita, (GGML), Ashraf Suryaningrat, amesema Mgodi huo utaendelea kuwekeza katika Ujuzi na Taaluma,biashara mahalia,Teknolojia ya Mnyororo wa Ugavi Uvumbuzi na Maendeleo Endelevu ya Jamii ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono safari ya kuelekea Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050.

GGML MGUU SAWA USHIRIKI DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050
Studio Narration JAMBO FM

GGML MGUU SAWA USHIRIKI DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

0:00 --:--

Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita, (GGML), Ashraf Suryaningrat, amesema Mgodi huo utaendelea kuwekeza katika Ujuzi na Taaluma,biashara mahalia,Teknolojia ya Mnyororo wa Ugavi Uvumbuzi na Maendeleo Endelevu ya Jamii ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono safari ya kuelekea Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050.

Ameyasema hayo Septemba 27,2026 kupitia Salamu za Mgodi alizozitoa katika Ufunguzi Maonesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini Geita ambayo yamefanyika kwa udhamini Mkuu wa Mgodi wa GGML kwa ushirikiano na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita,Manispaa ya Geita na Kuratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TANTRADE).

“Kwa niaba ya Anglo Gold Ashanti ninashukuru sana kushiriki hapa siku ya leo na ninasikia fahari tunapoianza safari ya dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, ushirikiano baina ya serikali,sekta binafsi wadau pamoja na jumuiya zinaoishi kando kando ya maeneo ya uchimbaji unachangia kwa kiasi kikubwa katika maelengo tuliyojiwekea kufikia dira ya Taifa ya Maendeleo 2050”amesema Suryaningrat

Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita, (GGML), Ashraf Suryaningrat akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Maonesho ya Teknolojia ya Madini Geita.Picha na Ibrahim Rojala

Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, Chacha Wambura kupitia uzinduzi wa maonesho hayo amesema miongoni mwa changamoto inayowasumbua wachimbaji wadogo wa madini mkoani Geita ni pamoja na utozaji kodi mara mbili (Double Taxation).

Kutokana na uwepo wa changamoto hiyo,ameiomba wizara ya madini Mbunge huyo amemuomba kuingilia kati suala hilo akidai kuwa limekuwa likiwarudisha nyuma wachimbaji wadogo wa madini. Pia, ameiomba Serikali kutumia asilimia za makusanyo ya mapato yatokanayo na sekta ya Madini kama ilivyoelekezwa katika Bajeti ya Wizara hiyo ya mwaka 2026/2027, kufanya utafiti wa maeneo ya migodi ambayo tayari yamekatiwa leseni ili kuwaruhusu wachimbaji kuanza shughuli zao.

Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini,Mhandisi Chacha Wambura akitoa salamu za Mbunge katika Uzinduzi wa Maonesho ya Tisa ya Tenknolojia ya Madini Geita.

Kwa upande wake,Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) ambao ni waratibu wa maonesho hayo,Fred Lihundi amesema mchango wa sekta ya madinikatika kukuza uchumiwa nnnchi umeendelea kuimarika ambapo kwa mujibu wa Takwimu za Benki kuu ya Tanzania(BOT),zilizoishia mwezi Juni,mauzo ya Madini yalifikia wastani wa Shilingi Trilioni 7.78 wakati mauzo yamwaka mzima wa 2025 mauzo yalikuwa ni Trilioni 11.7.

“Ukilinganisha na mwaka wa 2021, ambao serikali ya awamu hii ilikuwa inaingia madarakani,mauzo ya mwaka mzima yalikuwa shilingi Trilioni 7.2,Mheshimiwa Mgeni rasmi hii maana yake kwamba katika kipindi cha miaka mitano,mauzo ya mwaka mzima sasa tunayafikia kwa miezi sita tu”amesema Lihundi

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE,Fred Lihundi ambao ni waratibu wa maonesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini Geita, akizungumza kuhusu mafaniko yaliyopatikana nchini kupitia mauzo ya madini.

Katika salamu za mkoa,Mkuu wa mkoa wa Geita Alexander Mnyeti,ameiomba wizara ya madini kuona namna ya kushirikiana katika kutatua migogoro kati yawamilikiwa leseni za uchimbaji mdogo na wamilikiwa wa mashamba.

“Eneo hili lina utitiri wa migogoro kati ya wachimbaji na wamiliki wa mashamba,nawaombeni sana watu wa wizara ya madini jambo hili mlichukulie kwa uzito wake kama ambavyo waheshimiwa wabunge wamesema,jambo hili ni kero kubwa na kama serikali hatuwezi kulifumbia macho”amesema RC Mnyeti

Mkuu wa mkoa wa Geita Alexander Pastory Mnyeti akitoa salamu za Mkoa katika uzinduzi wa Maonesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini Geita.

Akizindua maonesho hayo,Naibu Waziri wa Madini Steven Kiruswa amewakumbusha wachimbaji wadogo wa madini umuhimu wa kuzingatia sheria inayoruhusu raia wa kigeni kutoa msaada wa kiufundi katika shughuli za uchimbaji,(Technical Support Assistance), badala ya kukabidhi leseni zao na kuwaacha wageni kuendesha shughuli za uchimbaji kama ambavyo wanafanya baadhi ya wachimbaji nchini.

Naibu Waziri wa Madini Steven Kiruswa akihutubia hadhira iliyojitokeza katika Uzinduzi wa Maonesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini Mkoa wa Geita.

Kuhusiana na changamoto ya migogoro kati ya wamiliki wa leseni za uchimbaji na wenye mashamba ameeleza kuwa serikali imekuwa ikisisitiza umuhimu wa pande zote mbili kukaa pamoja na kuangalia namna bora ya utendaji wenye kuzinufaisha pande zote,akiahidi kuwa wizara hiyo pia itahakikisha changamoto yaiutozwaji wa kodi mara mbili kwa wachimbaji wadogo inatatuliwa.

 

Mwonekano wa Viwanja Vya Maonesho vya Dkt.Samia Suluhu Hassan,kata ya Bomba mbili halmashauri ya Manispaa ya Geita,eneo ambalo Maonesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini Geita yanaendelea hadi Oktoba 3,2026.

Maonyesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini yalioanza Septemba 23 na kuzinduliwa rasmi Septemba 27,2026 yameshirikisha wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi wapatao 765,yakiwa na kauli mbiu isemayo;Madini ni Utajiri,Tuwajibike kwa pamoja Kufikia dira ya Taifa 2050.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.