Skip to main content

GEITA: WASHAURIWA KUFANYA KAZI KWA UWAZI, KUZINGATIA KANUNI

Na Ibrahim Rojala - Geita.

GEITA: WASHAURIWA KUFANYA KAZI KWA UWAZI, KUZINGATIA KANUNI

Na Ibrahim Rojala - Geita.

Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali yaliyopo ndani yaHalmashauri ya wilaya ya Geita kupitia wakurugenzi wao yameshauriwa kufanya kazi kwa uwazi, weledi na kuzingatia kanuni na sheria za nchi pamoja na katiba za mashirika husika yanapotekeleza kazi zake ndani ya jamii.

Hayo yameelezwa na Kaimu Katibu Tawala wilaya ya Geita, Bi. Leminatha Mbegete katika kikao kazi kilichoyakutanisha mashirika yanayopatikana ndani ya wilaya ya Geita kwa lengo la kujadili namna ya kufanya kazi kwa ushirikianondani ya  jamii ambapo pia ametoa wito kwa mashirika hayo kuwasilisha taarifa zao serikalini kwa wakati.

“Taarifa ndio imebebea kipi kinafanyika kwenye shirika,taarifa imebeba utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo inafanyika kupitia shirika lkwahiyo kupitia kikao hiki niwaombe tuwe tunatoa taarifa kwa wakati sahihi,” ameeleza Bi. Leminatha.

Aidha amesisitiza ushirikiano kati ya mashirika hayo na viongozi wa serikali za mitaa ambao ndio wenye uelewa wa mbinu mbalimbali zinazotumika kuwakusanya watu katika maeneo yao ya kiutawala hatua itakayoyarahisishia mashirika hayo utekelezaji wa kazi zake, akiyataka kuzingatia kanuni sheria na taratibu za nchi na katiba za mashirika husika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) Mkoa Geita, Paulina Alex Majogoro, ameyataka mashirika hayo kufanya kazi kwa kuzingatia maono waliyojiwekea ili kufanikiwa, ikiwemo kupata fedha za wahisani na kuongeza kuwa mashirika hayawezi kupata kutoka kwa  wadhamini kama yatakuwa hayajajikita katika kazi maalumu.

“Ili pia uweze kumshawishi mfadhili aweze kukusaidia lazima usimame kwenye maono yako,lazima usimame kwenye misingi yako,nina maana ya mission na vision,shirika kama la NELICO haliwezi kufanya kila kitu,lazima uchague maeneo ambayo wewe ni expert una ujuzi nayo,unaweza ukafanya kwa ubora zaidi,maeneo mengine uwaachie wengine,” amebainisha Bi. Majogolo

Naye Afisa Miradi wa Shirika la Solidaridad, Victor Kayombo, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano na kwamba kwa kufanya hivyo kutasaidia mashirika yao kupunguza gharama kubwa katika kutekeleza baadhi ya mambo.

“Ushirikiano ni jambo muhimu sana,ni jambo zuri kwasababu mashirika kushirikiana kunapunguza gharama ya uendeshaji kwasababu unaweza kukuta kitu unashindwa kukifanya wewe kumbe rasilimali hiyo mtu mwingine anayo,unaweza kumtafuta mkufunzi wa jambo ambalo unafikiri haliwezekani kwako lakini kumbe mwenzako tu jirani yako analo na analifanya kwa ufanisi mkubwa sana bila gharama kubwa,” ameeleza Kayombo.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) Wilaya Geita, Ayoub Bwanamadi, amesema kikao hicho kimelenga kuwayakutanisha mashirika hayo ili kujadili mafanikio na changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa shughuli zao ndani ya jamii katika wilaya ya Geita.

“Tumetumia fursa hii ya kikao cha leo kuweza kukumbushana  katika suala zima la utumaji wa taarifa kama vile  zinavyotakikwa kwa kila robo lakini vile vile pia kutengeneza mahusiano na mashirikiano mazuri na serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia idara zake za kisekta ndani ya halmashauri mbalimbali zilizopo,” amedokeza Bwanamadi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.