Skip to main content

GEITA: WANANCHI ZAIDI YA 24,000 KUNUFAIKA NA MARADI WA MAJI KAKOLA

Na Ibrahim Rojala, Nyang'hwale - Geita.

GEITA:  WANANCHI ZAIDI YA 24,000 KUNUFAIKA NA MARADI WA MAJI KAKOLA

Na Ibrahim Rojala, Nyang'hwale - Geita.

Zaidi ya wananchi 24,000 wa vijiji 6 katika Kata ya Kakola, Wilaya ya Nyang'hwale wanatarajiwa kunufaika na mradi wa maji wa Shilingi Milioni 984 unaotekelezwa na RUWASA.

Waziri wa Madini, Antony Mavunde ametembelea na kuzindua mradi huo ambao unatarajiwa kukamilika Septemba 2026 ambapo Chanzo cha mradi ni maji ya Ziwa Victoria kupitia kisima chenye urefu wa mita 90 chenye uwezo wa kuzalisha lita 7,840 kwa saa.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyangalamila, Mavunde amewaomba wananchi kulinda miundombinu hiyo ili mradi udumu na kutumika  kwa muda mrefu.

“Tutahakikisha tunasimamia ipaasavyo miradi mingi ya maji pembzoni mwa ziwa Viktoria ili wananchi wengi waweze kupata maji,niko hapa kwenye ardhi ya Nyangalamila nimefungua maji,nyinyi ni mashahidi mmeona,maji sasa yanakwenda kupatikana ya uhakika”ameeleza waziri Mavunde.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella amesema mradi huo utahudumia vijiji vya Iseni, Nyangalamila, Kabiga, Nwiga, Kasibuya na Nyamikonze.

Wananchi wa Kata ya Kakola wameishukuru Serikali kwa jitihada za kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.