Na Afarah Suleiman, Mbulu - Manyara.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Michael Semindu Amepokea gari jipya la kuzima moto,hatua inayokuja baada ya muda mrefu kuto kuwepo kwa chombo hicho, hali iliyopelekea wananchi kukosa huduma hiyo muhimu.
Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Semindu, amesema gari hilo litakuwa msaada mkubwa katika kukabiliana na majanga ya moto yanapotokea, na hivyo kuongeza usalama wa maisha na mali za wananchi.

Aidha, Semindu ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha huduma za kijamii na kusogeza huduma muhimu karibu na wananchi.
Kwa upande wake, Mkaguzi Msaidizi wa Zimamoto Wilaya ya Mbulu, Zablon Mangare amesema, ujio wa gari hilo utarahisisha kwa kiasi kikubwa utendaji kazi wa zimamoto wilayani humo. Pia amewahimiza wananchi kutumia huduma za zimamoto kwa usahihi na kutoa taarifa mapema pindi majanga ya moto yanapotokea.


Discussion
Reader comments
0 contributions