Duniani kuna matukio mengi ya vifo vya kustaajabisha katika historia, ambayo ukiyatafakari ni lazima utabaki na maswali ya kutosha bila majibu.
Leo nimekuandalia matukio saba ambayo yalitikisa Dunia kwa nyakati zake, kiasi yamebaki kama alama kihistoria nikianza na la kwanza ambalo litakuacha mdomo wazi.
1. Black Death (1347 - 1351) - Ulaya nzima.
H8vi vilikuwa ni vifo vya ajabu na vya haraka sana, kwani watu milioni 75 hadi 200 walikufa ndani ya miaka 4 tu.
Wanasimulia kwamba Kijiji kizima kingeamka asubuhi na kukuta watu wote wamekufa wakiwa na madoa meusi mwilini.
Chanzo hadi leo kinajadiliwa kwamba hawajajua shida ilikuwa nini je? ni panya? bakteria ama nini?
Hii ilikuwa ni huko Venice, London na Paris.
2. Mlima Vesuvius - Pompeii, Italia (79 AD).
Hapa historia inaonesha kuwa Mji mzima wa watu 16,000 ulikufa ndani ya masaa 24 tu.
Hii ilitokana na Volcano kulipuka, majivu moto ya 400°C yaliwafunika wakiwa hai .

Tukio hili lilitokea wakati wengine walikuwa wanakula, wengine wamelala na kut8kana na volcano hiyo Miili yao ilibaki kama sanamu hadi leo.
3. Tunguska, Siberia - Urusi (1908).
Mlipuko mkubwa kuliko bomu la atomiki mara 1000, uliharibu msitu wa ukubwa wa Mkoa wa Dar es Salaam yote.
Hakuna mtu aliyekufa papo hapo kwa sababu kulikuwa porini, lakini wanyama na miti milioni 80 ililala chini ndani ya sekunde moja.

Watu hadi leo hawajui kama ni meteor, UFO au nini na bado watafiti hawajaibuka na jibu la moja kwa moja nini hada kilijiri.
4. Dyatlov Pass - Milima ya Ural, Urusi (1959).
Wapandaji milima 9 ambao walikuwa ni wanafunzi mahiri walikufa kwa njia ya kutatanisha.
Hema yao ilikatwa kutoka ndani, walikimbia kwenye theluji ya -30°C bila viatu, lakini walikutwa wengine macho yametolewa, ulimi umekatwa, mbavu zimevunjwa kama gari limewagonga.

Hakuna aliyeelewa nini kilitokea hadi leo, na hulo limebaki kuwa ni fumbo.
5. Kijiji cha Roanoke - Marekani (1587).
Hapa Watu 115 waliowekwa kama koloni la kwanza la Waingereza Marekani walipotea usiku mmoja.
Walipoenda kuwatafuta, walikuta kijiji kipo tupu, chakula kipo mezani bado moto unawaka na neno moja tu limeandikwa kwenye mti: "CROATOAN".

Lakini cha kushangaza hakukuwa na maiti, hakuna damu wala ishara ya purukushani, yaani ni kama vile watu waliondoka wote na kuacha kila kitu kwa mpangilio kama watarudi baadaye.
6. Spanish Flu (1918-1920) - Dunia nzima.
Vifo vya ajabu zaidi kuwahi kutokea vilionekana hapa - watu vijana wenye afya waliamka asubuhi wako sawa, lakini jioni wakafariki.

Kiujumla Watu milioni 50 hadi 100 walikufa, sababu ikiwa haijulikani maana wanasema katika kambi za jeshi, askari angepiga chafya asubuhi na jioni wakakuta amekufa.
7. Lake Nyos - Cameroon, Afrika (1986).
Ziwa la kimya kimya, hapa usiku mmoja lilitoa gesi ya CO2 yenye sumu na kuua watu 1,746 na wanyama 3,500 waliolala ndani ya kilomita 25.
Hakuna mlipuko, hakuna kelele - watu waliamka asubuhi na kukuta majirani wote wamekufa wakiwa kitandani wamelala.

Hakika Dunia ina mambo ya kustaajabisha.
Discussion
Reader comments
0 contributions