Muigizaji wa Kisomali, Barkhad Abdi amekula matunda ya kazi yake baada ya kulipwa Dola 65,000 ya uigizaji wa filamu yake ya kwanza ya Captain Phillips.
Licha ya kupata malipo hayo, Barkhad 'hakuvimba' bali alirudi kuuza simu za mkononi kwenye duka la kaka yake huko Minneapolis, Marekani, kazi ambayo amekuwa akifanya nje ya uigizaji.

Abdi lizaliwa Mogadishu, Somalia,na baadaye alihamia Marekani yeye na familia yake akiwa na umri wa miaka 14.
Kabla ya kuingia Hollywood, alifanya kazi kama dereva wa limousine na biqshara ya kuuza simu za mkononi.

Maisha yake yalibadilika ghafla alipochaguliwa kuigiza kama Muse, kiongozi wa maharamia wa Kisomali katika filamu ya mwaka 2013 ya Captain Phillips.
Filamu hiyo iliigizwa ikijiegemeza katika tukio la kweli la kutekwa kwa meli ya mizigo ya Maersk Alabama mwaka 2009.

Licha ya kutokuwa na uzoefu wowote wa kuigiza filamu hapo awali, Abdi alitoa uigizaji uliompatia uteuzi wa Tuzo ya Academy (Oscar) ya Muigizaji Bora wa kusaidia mwaka 2014.
Abdi pia alishinda Tuzo ya BAFTA ya Muigizaji Bora wa Kusaidia mwaka huo huo wa 2014.
Discussion
Reader comments
0 contributions