Skip to main content

FAINALI MAYEYE CUP YAINGIA DOSARI KIGOMA

Fainali ya ligi ya Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Kiza Hussein Mayeye 'Mayeye CUP' 2026, imeshindwa kutamatika baada ya kutokea sintofahamu ya kikanuni katika mchezo huo uliotakiwa kufanyika katika uwanja wa tarafa ya Mwandiga Halmashauri ya Wilaya Kigoma ukizikutanisha Mwandiga United dhidi ya Majengo Sokoni ulisitishwa dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza.

FAINALI MAYEYE CUP YAINGIA DOSARI KIGOMA
Studio Narration JAMBO FM

FAINALI MAYEYE CUP YAINGIA DOSARI KIGOMA

0:00 --:--

Fainali ya ligi ya Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Kiza Hussein Mayeye 'Mayeye CUP' 2026, imeshindwa kutamatika baada ya kutokea sintofahamu ya kikanuni katika mchezo huo uliotakiwa kufanyika katika uwanja wa tarafa ya Mwandiga Halmashauri ya Wilaya Kigoma ukizikutanisha Mwandiga United dhidi ya Majengo Sokoni ulisitishwa dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza.

Akizungumza na waandishi, Katibu wa chama cha soka Wilaya ya Kigoma, Dumango Yahya, amesema mgogoro umemhusisha mchezaji wa Mwandiga United anayedaiwa kuchezea timu nyingine tofauti katika mashindano hayo kabla ya fainali, jambo ambalo ni kinyume cha kanuni za mashindano.

Muonekano wa kombe lililotakiwa kukabidhiwa kwa mshindi wa fainali hiyo.

Kwa upande wake, Kocha Msaidizi wa Mwandiga United, Mussa Jumanne Ramadhani, amekanusha madai hayo akisema mchezaji huyo hakucheza mchezo wowote na timu nyingine, bali wapinzani wao walimfuata na yeye akawakataa, ndipo chanzo cha vurugu hizo.

Naye Kocha wa Majengo Sokoni, Maulid Ally, amesema wao walimfuata awali kocha wa mchezaji huyo kutoka Timu ya Kasaka na akakiri kumchezesha mchezaji huyo katika mashindano hayo.

Kamati ya mashindano imesema itakaa kwa dharura kupitia kanuni na taarifa muhimu ili kujiridhisha na kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu hatima ya fainali hiyo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.