Hali ya hofu imetawala katika kitovu cha mji wa tigray kaskazini mwa Ethiopia baada ya wanamgambo wanaotajwa kuungwa mkono na serikali kuuteka mji wa Alamata, kusini mwa mekelle.
Duru kutoka nchini Ethiopia zimeripoti kutapakaa kwa video mitandaoni zinazoonyesha vikosi vya wanamgambo hao na jeshi la serikali vikiwa na silaha za kutuliza ghasia huku giza la mawasiliano likitanda kutokana na kukatwa kwa huduma za simu na internet.

hata hivyo katika taarifa ya Jeshi la serikali ya Ethiopia imearifu kuwa vikosi hivyo vimefanikiwa kuweka chini ya udhibiti huo.
Hatua hiyo inakuja baada ya mapigano makali yaliyoibuka mwanzoni mwa juma lililoisha na kuathiri zaidi maeneo ya tigray pamoja na Amhara.

Hata hivyo mapema jumamosi sept.26 ya mwaka huu umoja wa mataifa kupitia kamishna mkuu wa haki za binadamu Volker türk alionya vikali kuhusu hatari inayowakabili raia kutokana na kushamiri kwa mapigano kati ya wanajeshi wa serikali ya Ethiopia na wapiganaji wa Tplf huko Tigray.

Kadharika Kamanda mkuu wa Jeshi la Ethiopia, Berhanu Jula, amezishutumu serikali za eritrea, sudan na misri kwa kuunga mkono waasi wa tplf wakati Eritrea na Sudan zikikanusha madai hayo.

vuguvugu la udhibiti mjini Tigray limeambatana na kukatwa kwa huduma za simu na intaneti kwa siku zipatazo 3 mfululizo tangu tarehe 25 sept.2026.
kwa mujibu wa umoja wa Mataifa, mamia ya maelfu ya wakazi wa tigray bado wasalia kuyahama makazi yao kutokana na athari za vita vya awali.
.
Discussion
Reader comments
0 contributions