Skip to main content

ENDELEENI NA SHUGHULI JULAI 7, TUMEJIPANGA KULINDA AMANI - SERIKALI

Serikali imewataka wafanyabiashara, wajasiriamali, waendesha bodaboda na bajaji pamoja na wananchi wote kuendelea na shughuli zao za kiuchumi kama kawaida Julai 7, 2026, ikisisitiza hakuna sababu ya kusitisha shughuli kwa kuhofia maandamano yaliyotangazwa kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kuimarisha amani na utulivu.

Rai hiyo imetolewa jana, Jumamosi Julai 4, 2026, na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, wakati wa mkutano uliojumuisha wajasiriamali, waendesha bodaboda, wamachinga, mama lishe na baba lishe wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Katika mkutano huo, uliofanyika viwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, ulidhuriwa na Naibu waziri wa Mambo ya Ndani, Ayoub Mohamed Mahmoud ambapo wajasiriamali hao waliwaeleza viongozi hao kuhusu msimamo wao wa kuendelea kulinda amani na kutokubali kutumiwa kisiasa.

“Kumekuwa na tabia ya kutangaza maandamano yasiyofuata sheria mara kwa mara. Kilichotokea Oktoba 29, 2025 hakitajirudia hapa nchini. Serikali imejipanga wakati wote kuwachukulia hatua wote watakaojaribu kuvuruga amani na utulivu wa nchi,” amesema Katambi.

Amesema lengo la wanaotangaza maandamano hayo ni kuvuruga amani na kuathiri shughuli za kiuchumi, jambo ambalo Serikali haitaliruhusu.

"Watu hawa wana lengo la kuondoa amani ili kudhoofisha uchumi wa nchi. Ndiyo maana wamekuwa wakipanga maandamano. Serikali haitakubali tena kujitokeza kwa matukio kama hayo," amesema.

Waziri huyo, amewahakikishia Watanzania kuwa hali ya usalama nchini iko imara na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama viko tayari kuhakikisha wananchi wanaendelea na shughuli zao bila hofu.

“Watanzania waendelee na shughuli zao kama kawaida. Serikali imejipanga kulinda usalama wa wananchi na mali zao wakati wote, hivyo hakuna sababu ya kuruhusu hofu inayosababishwa na watu wenye nia ovu,” amesema.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.