Skip to main content

ELIMU MATUMIZI YA NISHATI SAFI KWA MADIWANI ITIGI ITAFIKA NGAZI YA VIJIJI - SIMBA

Na Saulo Stephen - Singida.

ELIMU MATUMIZI YA NISHATI SAFI KWA MADIWANI ITIGI ITAFIKA NGAZI YA VIJIJI - SIMBA

Na Saulo Stephen - Singida.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Hussein Simba, ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Nishati kwa kuandaa mafunzo kwa madiwani kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia na faida zake, akisema elimu hiyo itasaidia kuwafikia wananchi hadi ngazi ya vijiji.

Simba ameyasema hayo baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku moja yaliyowakutanisha madiwani katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, yaliyolenga kuwajengea uelewa kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Amesema madiwani wamepokea mafunzo hayo kwa hamu kubwa, kutokana na kuwepo kwa maswali na maoni mengi kutoka kwa wananchi kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Kupitia vikao na mikutano mbalimbali, wataweza kuwafikishia wananchi elimu waliyoipata kuhusu matumizi sahihi ya nishati safi ya kupikia,” amesema Simba.

Kwa upande wake, Mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye ni Mjiolojia Mkuu kutoka Wizara ya Nishati, Ngelejwa Mgejwa, amesema Serikali imelenga kuhakikisha elimu kuhusu matumizi sahihi ya nishati safi ya kupikia inawafikia wananchi wengi zaidi kupitia viongozi wa ngazi za chini.

Amesema madiwani wana nafasi kubwa katika kufikisha ujumbe huo kwa wananchi kupitia vikao vya Halmashauri, Kata na vijiji, hivyo elimu waliyopewa inapaswa kutumika kuwahamasisha wananchi kuhusu umuhimu na faida za kutumia nishati safi ya kupikia.

Mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia, pamoja na kuhamasisha jamii kuachana na matumizi ya nishati zinazoweza kuwa na madhara kwa afya na mazingira.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.