Wakati mvua za el nino zikiripotiwa kuanza kunyesha katika baadhi ya Maeneo ya Africa kabla ya kufikia kilele chake mwezi Desemba, hofu kubwa imeendelea kutanda nchini Somalia juu ya usalama wa chakula na maisha ya raia.
Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu (ICRC) imetoa tahadhari kuwa wakulima nchini humo wanakabiliwa na hali ngumu ya mafuriko, sambamba na janga kubwa la njaa.

Nuh Adan, mkulima na kiongozi wa jamii katika eneo la Bayahaaw, ameeleza kuwa iwapo kingo za mto zitapasuka, athari zake katika sekta ya kilimo za eneo hilo zitadumu kwa miezi kadhaa.

Hata hivyo Somalia imekuwa ikiorodheshwa mara kwa mara na mashirika ya kimataifa kuwa ni miongoni mwa maeneo yaliyo katika hatari kubwa zaidi katika kipindi cha mzunguko wa mvua za El nino
Kwa mujibu wa takwimu za mwenendo wa hali ya hewa wa kidunia 2023 ulileta maafa makubwa, ukiwaathiri karibu watu milioni mbili na kuwafanya watu nusu milioni kukimbia makazi yao katika Taifa hilo
Mkuu wa ICRC nchini Somalia, Antoine Grand, alisema kuwa hivi sasa wamejipanga kuchukua hatua za haraka kuikabili mvua hiyo.
Discussion
Reader comments
0 contributions