Skip to main content

EBOLA: KENYA YATHIBITISHA KIFO CHA KWANZA, 28 WAHISIWA

Kenya imethibitisha kisa cha kwanza cha kifo cha maambukizi ya virusi vya Ebola nchini humo, Waziri wa Afya Aden Duale ametangaza leo jumanne kuingia kwa virusi hivyo kufuatia kifo cha raia wake.

EBOLA: KENYA YATHIBITISHA KIFO CHA KWANZA,  28 WAHISIWA
Studio Narration JAMBO FM

EBOLA: KENYA YATHIBITISHA KIFO CHA KWANZA, 28 WAHISIWA

0:00 --:--

Kenya imethibitisha kisa cha kwanza cha kifo cha maambukizi ya virusi vya Ebola nchini humo, Waziri wa Afya Aden Duale ametangaza leo jumanne kuingia kwa virusi hivyo kufuatia kifo cha raia wake.

Kwa mujibu wa taarifa za Waziri huyo alikuwa akiishi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kabla ya kuwasili nchini humo.

Raia huyo wa kiume, ambaye jina lake halijawekwa wazi inaarifiwa alianza kuugua takriban mwezi mmoja uliopita na alipata matibabu nchini DRC kabla ya kusafiri kwa njia ya barabara kuelekea jijini Kampala,Uganda, na kisha kupanda ndege kuelekea Nairobi tarehe 3 Oktoba, kulingana na Aden Duale Waziri wa Afya wa Kenya.

Waziri Duale aliongeza kuwa mgonjwa huyo alipimwa na kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo hatari, akieleza kuwa "kwa masikitiko makubwa alifariki dunia jana usiku majira ya saa tano na nusu usiku (11:30)."

Hata hivyo Serikali imeeleza kuwa tayari imebaini orodha ya watu 28 waliokuwa na mawasiliano ya ukaribu ya kijamii na marehemu, wakiwemo wanafamilia pamoja na wahudumu wa afya waliomhudumia.

Hiki kinakuwa kisa cha kwanza cha Ebola kurekodiwa nchini Kenya. Mapema mwaka huu,huku Serikali ya Kenya ikichukua hatua ya kupanga kujenga kituo cha matibabu ya Ebola katika Kituo cha Jeshi la Anga cha Laikipia (Laikipia Air Base), ikiwa ni takriban kilomita 200 kutoka Nairobi.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ilitangaza mlipuko wake wa 17 wa Ebola katikati ya mwezi Mei. Ugonjwa huo umeua zaidi ya watu 15,000 barani Afrika katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.

Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), hadi kufikia tarehe 2 Oktoba, watu 4,082 wameripotiwa kufariki dunia kati ya visa 8,463 tangu kuibuka kwa aina mpya ya virusi hivyo chapa ya Bundibugyo strain, ambayo hadi sasa haina chanjo wala matibabu maalum.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.