Takriban watu 57 wamebainika kuwa na mawasiliano na mgonjwa wa kwanza, aliyethibitishwa kuwa na maambukizi ya Ebola nchini Kenya.
Kufuatia hali hiyo, 10 kati ya hao 57 wamewekwa karantini, huku Wizara ya Afya ikiongeza kasi ya ufuatiliaji wa watu waliokutana na mgonjwa wa awali.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya anayesimamia Afya ya Umma, Mary Muthoni, amesema idadi ya watu wanaofuatiliwa huenda ikaongezeka.
Amesema, Maafisa wa Afya nchini humo, tayari wamepewa maelekezo ya kuwa katika hali ya tahadhari na kuhakikisha maambukizi yote yanayoshukiwa na Ebola yanashughulikiwa kwa haraka ipasavyo.
Discussion
Reader comments
0 contributions