Tanzania inatumia Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kama jukwaa la kuunganisha vipaumbele vyake vya maendeleo na mijadala ya kimataifa, huku ikitoa nafasi kwa nchi mbalimbali kujifunza uzoefu wa Tanzania katika maeneo ya amani, utawala, afya, ushiriki wa wanawake na maendeleo ya miundombinu.
Kupitia mkutano huo, Tanzania inalenga kutumia majadiliano na mikutano ya nchi mbalimbali kujenga ushirikiano, kubadilishana uzoefu na kuibua mawazo mapya yanayoweza kusaidia kuharakisha utekelezaji wa ajenda za maendeleo barani Afrika.

Mijadala hiyo pia inatoa fursa ya kuunganisha masuala ya kitaifa na ajenda za kimataifa, ikiwemo Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.
Kwa Tanzania, IPU 153 pia ni fursa ya kuonesha uzoefu na vipaumbele vya nchi mbele ya jumuiya ya kimataifa, huku ikisisitiza umuhimu wa amani kama msingi wa maendeleo, miundombinu inayowaunganisha wananchi na fursa, pamoja na kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika uongozi na maamuzi.
Mkutano huo unaofanyika Arusha Oktoba 5–9, 2026, unawakutanisha zaidi ya washiriki 2,000 kutoka mabunge 183 duniani.
Discussion
Reader comments
0 contributions