Skip to main content

DTK. SAMIA AMPOKEA RAIS WA MISRI EL-SISI IKULU DAR ES SALAAM

Rais Samia Suluhu Hassan, leo Julai 18, 2026 amempokea Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fattah El-Sisi aliyewasili Nchini kwa ziara ya Kitaifa.

DTK. SAMIA AMPOKEA RAIS WA MISRI EL-SISI IKULU DAR ES SALAAM

Rais Samia Suluhu Hassan, leo Julai 18, 2026 amempokea Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fattah El-Sisi aliyewasili Nchini kwa ziara ya Kitaifa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, baada ya mapokezi hayo viongozi hao watafanya mazungumzo rasmi yatakayolenga kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Misri pamoja na kupanua ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwamo biashara, uwekezaji, kilimo, nishati, maji, afya, elimu na miundombinu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fattah El-Sisi, Ikulu Jijini Dar es Salaam, Julai 18, 2026.

Kadhalika, Rais Samia na Rais El-Sisi watashiriki Jukwaa la Biashara la Tanzania na Misri litakalowakutanisha Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka mataifa hayo mawili kwa lengo la kujadili fursa za biashara na uwekezaji.

Ziara hiyo inatarajiwa kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo kati ya Tanzania na Misri na kufungua fursa mpya za biashara na uwekezaji kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.