Skip to main content

DOREFA WAAHIDI MAZINGIRA RAFIKI KWA TIMU ZINATOTUMIA UWANJA WA JAMHURI

Na Gideon Gregory - Dodoma.

DOREFA WAAHIDI MAZINGIRA RAFIKI KWA TIMU ZINATOTUMIA UWANJA WA JAMHURI

Na Gideon Gregory  - Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma (DOREFA), Aden Mohammed ameahidi kuweka mazingira rafiki kwa klabu zinazoutumia uwanja wa Jamhuri kama uwanja wa nyumbani.

Aden ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Mjumbe wa Kanda namba 4 inayojumisha Mikoa ya Singida, Dodoma, Shinyanga na Simiyu ametoa ahadi hiyo leo Machi 28,2026 wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma (DOREFA).

"Tunafurahi  kwa jinsi ambayo Mkoa wetu wa Dodoma umekuwa na timu nyingi za Ligi Kuu, Dodoma Jiji, Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons," amesema. 

Ameongeza kuwa Dorefa itaendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi ili klabu hizo ziendelee kuutumia uwanja wa Jamhuri kama uwanja wa nyumbani kwa kuhakikisha zinafanya vizuri," amesema. 

"Niwaahidi wana Dodoma, Dorefa itaendelea kuhakikisha soka linachezwa kuanzia ngazi ya chini mpaka ya juu lengo vipaji vizidi kuonekana," amesema Aden.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa zamani wa Soka Mkoa wa Dodoma (DOREFA), Nassoro Kipenzi ameshauri mambo matatu kwa Chama cha Soka Mkoani Dodoma ikiwemo kuhakikisha soka linachezwa wilayani.

Kipenzi ambaye aliiongoza Dorefa kwa miaka 8 kuanzia mwaka 2008-2016 na kumwachia Mulamu Ng'ambi ambaye aliongoza mpaka mwaka 2020 na kumwachia Mwenyekiti wa sasa Aden Mohammed.

"Nilienda Wilaya ya Chamwino kule nilikuta soka linachezwa sasa hii iwe kote soka lichezwe ili kutoa nafasi ya vipaji kuonekana," amesema Kipenzi.

Pia ameshauri kuendelea kuhakikisha inazilinda klabu za Dodoma Jiji inayoshiriki Ligi Kuu na Gunners inayoshiriki Championship kuhakikisha zinaendelea kufanya vizuri.

Katika mkutano huo wajumbe wamepitisha  Mpango kazi wa mwaka 2025-2026 wa Chama cha Soka Mkoani Dodoma.

Ambapo moja ya malengo ni kuhakikisha kunakuwa na ligi imara na yenye ushindani kwa vijana,kuendeleza mpira wa miguu kwa wanawake pamoja na kuendeleza ushirikiano na wadau wa Soka.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.