Skip to main content

DODOMA: WANANCHI WAAHIMIZWA UTAMADUNI KUPIMA AFYA MARA KWA MARA

Baadhi ya wananchi wa makundi mbalimbali, wakiwemo wafanyabiashara wa Soko la Machinga jijini Dodoma wamesema utolewaji wa huduma za afya mara kwa mara katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi ni muhimu kwani huwapatia fursa ya kufahamu hali zao na kusaidia wale wasiokuwa na uwezo kufuata huduma hizo hospitalini.

DODOMA: WANANCHI WAAHIMIZWA  UTAMADUNI KUPIMA AFYA MARA KWA MARA
Studio Narration JAMBO FM

DODOMA: WANANCHI WAAHIMIZWA UTAMADUNI KUPIMA AFYA MARA KWA...

0:00 --:--

Baadhi ya wananchi wa makundi mbalimbali, wakiwemo wafanyabiashara wa Soko la Machinga jijini Dodoma wamesema utolewaji wa huduma za afya mara kwa mara katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi ni muhimu kwani huwapatia fursa ya kufahamu hali zao na kusaidia wale wasiokuwa na uwezo kufuata huduma hizo hospitalini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Oktoba 8,2026 wakati wakipatiwa huduma za afya zinazotolewa kwa ushirikiano kati ya Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, wananchi hao wamesema huduma za aina hiyo zimekuwa na umuhimu mkubwa kwa jamii.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Profesa Abel Makubi amesema wananchi wanapaswa kuwa na utamaduni wa kupima afya zao, akieleza kuwa hatua hiyo inalenga kutoa elimu kuhusu namna ya kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ikiwemo kisukari, presha, magonjwa ya moyo na kansa, pamoja na afya ya akili.

"Wananchi watapatiwa elimu ya namna ya kudhibiti magonjwa hayo au kupunguza makali yake endapo watakuwa wamegundulika kuwa nayo,"amesema.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuzingatia kinga badala ya kusubiri hadi mtu anapougua huku akiwataka wananchi kujiunga na bima ya afya mapema, akieleza kuwa hatua hiyo itawasaidia kupata huduma pindi wanapougua au kupata ajali.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Misana Yango, amesema ushirikiano katika utoaji wa huduma hizo ni muhimu katika kuimarisha afya za wananchi na kuwafikia wale ambao wanaweza kuwa na changamoto ya kufika katika vituo vya afya.

Huduma hizo za afya zimeanza Oktoba 8, 2026 na zitaendelea hadi Oktoba 13, 2026 ambapo zinazotolewa bure na kuwapa wananchi fursa ya kufanyiwa uchunguzi na kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu afya zao.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.