Skip to main content

DKT. NETHO AMRITHI RASMI NDEJEMBI UBUNGE CHAMWINO

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Chamwino, Godfrey Mnyamale, amemtangaza Dkt. Netho Ndijina Ndilito wa CCM ndiye mshindi ambapo kati ya kura halali 86,590 zilizopigwa, amebeba kura 70,974 - sawa na asilimia 81.9, jambo linalotoa takwimu kwamba kati ya watu 10 waliopiga kura Chamwino, wanane walimpigia Dkt. Netho.

DKT. NETHO AMRITHI RASMI NDEJEMBI UBUNGE CHAMWINO

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Chamwino, Godfrey Mnyamale, amemtangaza Dkt. Netho Ndijina Ndilito wa CCM ndiye mshindi ambapo kati ya kura halali 86,590 zilizopigwa, amebeba kura 70,974 - sawa na asilimia 81.9, jambo linalotoa takwimu kwamba kati ya watu 10 waliopiga kura Chamwino, wanane walimpigia Dkt. Netho.

Dkt. Netho alikuwa akikabiliana na wagombea 16 kutoka vyama mbalimbali, lakini hakuna aliyemfikia hata karibu.

Aliyemfuata kwa mbali ni Philemon Nyakapala wa CHAUMMA aliyepata kura 10,315. Tofauti ni kura zaidi ya 60,000.

Uchaguzi huu haukuwa wa kupita, kwani kati ya wapiga kura 133,864 walioandikishwa, 87,329 walijitokeza kupiga kura sawa na asilimia 65.2 ambapo kura 739 zilikataliwa.

Mara tu baada ya kutangaza matokeo, Mnyamale alimkabidhi Dkt. Netho cheti cha ushindi wa ubunge, ambapo sherehe, vifijo na nderemo vilitawala.

Macho yote ni kwa Dkt. Netho ambaye anarithi nafasi iliyoachwa na Deogratius Ndejembi, ambaye aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.

Wananchi wa Chamwino wanamngojea aapishwe na kuanza kazi, huku ahadi alizotoa mshindi huyo wakati wa kampeni zikitqrajiwa kuwa ndio wakati wa kuzitekeleza.

Matokeo Kamili ya Wagombea Wengine ni kama ifuatavyo-,

2. Philemon Nyakapala (CHAUMMA) - 10,315

3. Exavery Mapunda (AAFP) - 1,042

4. Shabani Kirita (SAU) - 843

5. Mohamed Mnyalape (NLD) - 562

6. Christina Denis Sembuche (NCCR-MAGEUZI) - 483

7. Samwel Mazengo (UMD) - 476

8. Rahel George (NRA) - 418

9. Jeremia Alexander (ADC) - 351

10. Judith Ngolola (ADA-TADEA) - 213

11. Lailath Mbuta (TLP) - 197

12. Karunde Juma (CCK) - 196

13. Baraka Machumu (MAKINI) - 182

14. Nasma Hamisi (UDP) - 173

15. Runna Karya (UPDP) - 104

16. Damaly Richard (DP) - 61

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.