Skip to main content

MAKAMU WA RAIS DKT. NCHIMBI AJIUZULU

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Emmanuel Nchimbi, amemwandikia Rais Samia Suluhu Hassan, barua ya kujiuzulu wadhifa huo, miezi michache baada ya kutoa kauli mbalimbali zenye utata.

MAKAMU WA RAIS DKT. NCHIMBI AJIUZULU

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Emmanuel Nchimbi, amemwandikia Rais Samia Suluhu Hassan, barua ya kujiuzulu wadhifa huo, miezi michache baada ya kutoa kauli mbalimbali zenye utata.

Kabla ya taarifa hiyo, Dk Nchimbi kwa nyakati tofauti amekuwa akiibua kauli zinazoleta utata, ikiwemo ile aliyowataka Watanzania wapambane kuipata Katiba Mpya, ilhali ajenda hiyo tayari ilishawekewa utaratibu ndani ya chama chake cha CCM na hata kuwa katika Ilani ya chama hicho.

Kauli hiyo iliibua sintofahamu hata ndani ya CCM. Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, Fadhili Maganya, aliijibu kwa kuhoji, anayewashinikiza Watanzania wapambane kupata Katiba Mpya, anataka wapambane na nani?

Dkt. Emmanuel Nchimbi.

Sambamba na kauli ya Maganya, Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi, Mohamed Simai Said, aliwahi kusema ndani ya Serikali kuna kiongozi msaliti akimwita ‘Yuda’ kwa kile alichosisitiza, anakinzana na mwelekeo na dhamira ya Serikali.

Mienendo hiyo, ilimwibua Mwanasiasa mkongwe, John Shibuda ambaye Agosti 23, 2026 alizungumza na vyombo vya habari, akimsihi Dk Nchimbi ajiuzulu kutokana na mwenendo wake unaokwenda kinyume na mwelekeo wa Serikali

Dk Nchimbi ametoa taarifa ya kuandika barua ya kujiuzulu na kusambaza katika kurasa za mitandao yake ya kijamii leo, Agosti 25, 2026.

Katika barua yake, ameandika atajiuzulu wadhifa huo kuanzia Septemba 4, 2026 akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na wananchi kwa kipindi alichoongoza.

Amesema, kujiuzulu kwake kutaanza rasmi Septemba 4, 2026, akieleza kuwa amefanya uamuzi huo kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa ya Nchimbi imeeleza kuwa Agosti 27, 2025 alimuahidi Rais Samia kuwa angemsaidia yeye na taifa kwa uwezo wake wote na kwa uaminifu, huku akiahidi pia kuachia nafasi hiyo endapo Rais angeona anahitaji Makamu mwingine wa Rais.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.