Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Septemba 30, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa madereva wa mabasi na malori nchini.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Oysterbay, jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, Viongozi wamekubali kusitisha mgomo uliodumu kwa siku mbili, ili huduma za usafiri ziendelee.
Katika kikao hicho, Serikali imeonesha utayari wa kusikiliza na kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili madereva.

Discussion
Reader comments
0 contributions