Skip to main content

DKT. MBOYA AZINDUA MRADI WA MSINGITek TABORA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dkt. John Rogath Mboya, amezindua rasmi Mradi wa MsingiTek unaolenga kuboresha stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa wanafunzi wa Darasa la Kwanza hadi la Tatu kupitia matumizi ya vishikwambi.

DKT. MBOYA AZINDUA MRADI WA MSINGITek  TABORA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dkt. John Rogath Mboya, amezindua rasmi Mradi wa MsingiTek unaolenga kuboresha stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa wanafunzi wa Darasa la Kwanza hadi la Tatu kupitia matumizi ya vishikwambi. 

Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Mtemi Isike Mwanakiyungi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, ukihusisha viongozi wa elimu pamoja na wadau wa sekta hiyo. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dkt. Mboya amesema mradi huo unaotekelezwa na Imagine Worldwide kwa kushirikiana na TEDI ni hatua muhimu katika kutafsiri kwa vitendo ajenda ya kitaifa ya kuimarisha umahiri wa KKK kwa watoto. 

Amesema stadi hizo ni msingi wa ujifunzaji wa mtoto, hivyo matumizi ya sayansi na teknolojia yanapaswa kuelekezwa kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya kujifunza mapema.

 Amesema MsingiTek inakwenda sambamba na Mkakati wa Kitaifa wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu uliozinduliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Januari 29, 2026. Kwa mujibu wa Dkt. Mboya, mpango huo unaunga mkono Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Ajenda ya Afrika 2063 na Lengo la Nne la Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG 4) linalosisitiza elimu bora na jumuishi kwa wote. 

Akiwasilisha taarifa ya mradi, Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwl. Upendo Rweyemamu, amesema MsingiTek inatarajia kupanua wigo zaidi na kufikia zaidi ya shule 200 katika wilaya za Sikonge, Uyui na Kaliua ifikapo Mei 2027.

Dkt. Mboya amewaelekeza Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, Maafisa Elimu na viongozi wengine wa elimu kusimamia mahudhurio ya wanafunzi, matumizi sahihi ya vifaa vya kidijitali, uwezeshaji wa walimu na uboreshaji wa miundombinu ili kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekosa fursa hiyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Gasto Andrea Rwambano, ameishukuru Serikali na wadau wakiwemo Imagine Worldwide kwa kuleta mradi huo unaowawezesha watoto kumudu stadi za KKK.

Pia ameomba ongezeko la bajeti na wigo wa mradi huo ili uweze kuwafikia watoto wengi zaidi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.