Lokesheni ni London nchini Uingereza, hapo kulikuwa na mwanamke mmoja akifahamika kwa jina la Dkt. Margaret McCollum.
Yeye kila siku alikuwa akienda kwenye kituo cha treni ya chini ya ardhi na kuketi mahali, ili kusikiliza tangazo lililorekodiwa na mumewe, Oswald Lawrence, aliyefariki 2003.
Ulikuwa ni utaratibu wa Margaret, kujitafutia faraja ya moyo, kwa kumsikiliza mumewe kupitia sauti na kujihisi yu karibu naye.

Baada ya miaka mingi kupita, kutokana na mabadiliko ya nyakati, tangazo lilibadilishwa na Margaret alifadhaika sana.
Hata hivyo, alifanya mipango na akaomba apatiwe tangazo hilo, ili akaendelee kusikiliza sauti ya mumewe nyumbani kwake.

Lakini, kwa kutambua historia iliyo nyuma ya tangazo hilo, mamlaka ya kituo cha treni iliamua kurejesha tangazo hilo katika kituo cha treni jirani na nyumba anayoishi Margaret.
Walilenga kumpatia furaha yeye binafsi na kuwakumbusha abiria wengine kuwa mapenzi ya kweli yangalipo.
Discussion
Reader comments
0 contributions