Mbunge wa Kundi la vyuo la vyuo vikuu ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya ustawi na mendeleo ya jamii Dkt.Regina Malima amewataka wafanyabiashara wadogo wenye biashara zinazofanana kuunda vikundi na kurasimisha biashara zao ili waweze kupata tenda mbalimbali katika taasisi na sekta mbalimbali za serikali.
Dkt.Malima ameysema hayo wakati wa semina wa kuwajengea uwezo Wanawake,Vijana na watu wenyeulemavu iliyofanyika kata ya Nyahanga manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.
Amesema kuwa ni vigumu kufanikiwa kama unafanya kazi peke yako,lakini mkijiunga na mkaingia kwenye mfumo wa serikali mkiwa na vikundi vya watu watano watano ni rahisi kufahamika na kuwa na uwezekano wa kukopesheka ili kuongeza mtaji na kuendesha shughuli kwa Pamoja.
“Katika shughuli za ujasiliamali unaweza kufanikiwa ukiwa pekeyako lakini mnapounda kikundi itakuwa rahisi kufanikiwa kwani mnaweza pata tenda mbalimbali za sekta binafsi na taasisi za serikali,baada ya kusajili vikundi vyetu tunaviingiza katika mfumo wa serikali,hii inakuwa rahisi kupata mikopo na kupata tenda serikalini” Amesema Dkt.Malima.
Katika hatua nyingine Dkt.Malima amesisitiza uundaji wa vikundi uendane na kufahamiana kwa mtu mmoja mmoja ili ufanisi wa kikundi uwe ulionyooka na kila kikundi kiwe na uongozi na serikali ya mtaa ivifahamu vikundi hivyo na wapi wana kikundi wanapatikana.
“Tunapotengeneza vikundi lazima tuzingatie kuwa tunafahamiana mtu mmoja mmoja,ili vikundi vyetu viwe hai na tuwe tunafahamiana ili kuleta ustawi wa vikundi vyetu,lakini pia uongozi wa kata husika lazima uvifahamu vikundi hivi na mahali wapi wanakikundi wanapatikana” Ameongeza Dkt.Malima.
Sambamba na hayo Dkt.Malima ameliomba Shirika la maendeleo ya viwanda vidogo (SIDO) mkoa wa Shinyanga kuandaa mafunzo ya vitendo kwa wajasiliamali wadogo ambao watajifunza kutengeneza sabuni,batiki na keki ili wajasiliamali wawe na uwezo wa kutengeneza bidhaa hizo.
“Niwaombe ndugu zetu wa SIDO waje waandae mafunzo ya vitendo kwa wajasiliamali wadogo hasa mafunzo ya kutengeneza Sabuni za miche na sabuni za maji,Lakini pia hata utengenzaji wa batiki na keki,hii itawasaidia wajasiliamali kuwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza vitu hivyo” Amesisitiza Dkt.Malima.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya Jamii manispaa ya Kahama ambaye ni Mratibu wa Mikopo ya 10% Bi Hilda Boniphace amesema kuwa mikopo ya 10% inapatikana halmashauri ila kwa wote ambao wanahitaji na wanabiashara kubwa ni lazima wawe na leseni za biashara na wale wanaotaka mikopo ya pikipiki na bajaji sharti wawe na leseni ya udereva.
“Mikopo bado ipo halmashauri kikubwa zingatieni muwe kwenye kikundi cha watu watano,na wale ambao wanataka mkopo ila wana biashara kubwa ni lazima wawe na leseni ya biashara na kwa wale ambao wanahitaji mkopo wa pikipiki na bajaji lazima wawe na leseni ya udereva ndipo waweze kupata mikopo hii” Amesema Bi.Hilda.
Nao baadhi ya washiriki wa semina hiyo Isack Madirisha na Rozy Sultani wamesema kuwa semina hiyo imewapa mwanga wa jinsi ya kudhibiti matumizi ya fedha za mikopo Pamoja na kufahamu jinsi ya kujiunga na vikundi ili kuweza kupata mikopo ya 10% ikiwa ni Pamoja na namna ya kuanzisha biashara na kuirasimisha.
“Nimefurahia sana semina hii kwani imeweza kunipa mwanga wa jinsi gani ya kudhibiti mtumizi ya mikopo lakini pia tumefahamu namna ya kujiunga na vikundi,sambamba na hayo tumejifunza namna ya kuanzisha biashara na jinsi ya kuirasimisha biashara na kupata usajili” Wamesema Washiriki hao.
Semina hiyo imeshirikisha iliyofanyika kaya ya Nyahanga manispaa ya Kahama imeshirikisha kundi la vijana,Wanawake na watu wenye ulemavu kutoka maeneo mbalimbali ya manispaa ya Kahama.
Discussion
Reader comments
0 contributions